• HABARI MPYA

  Wednesday, December 12, 2018

  CAVANI, NEYMAR NA MBAPPE WOTE WAFUNGA PSG YAUA 4-1 UGENINI

  Edinson Cavani (kushoto) akiwatazama washambuliaji wenzake, Kylian Mbappe na Neymar wakishangilia baadsa ya wote kuifungia Paris Saint-Germain katika ushindi wa 4-1 dhidi ya wenyeji, Red Star Belgrade kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Rajko Mitic mjini Belgrade.  Cavani alifunga dakika ya tisa, Neymar dakika ya 40 na Mbappe dakika ya 90 na ushei, wakati bao lingine la PSG lilifungwa na Marcos Aoas Correa 'Marquinhos' dakika ya 74, huku la Red Star Belgrade likifungwa na Marko Gobeljic dakika ya 56.
  Kwa matokeo hayo, PSG inamaliza kileleni mwa kundi hilo kwa pointi zake 11, ikifuatiwa na Liverpool yenye pointi tisa na zote zinafuzu hatua ya 16 Bora zikizipiku Napoli iliyomaliza na pointi tisa pia na Red Star Belgrade pointi nne 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAVANI, NEYMAR NA MBAPPE WOTE WAFUNGA PSG YAUA 4-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top