• HABARI MPYA

  Sunday, December 09, 2018

  SAMATTA AFUNGA BAO LA KUONGOZA KRC GENK YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA KORTRIJK KATIKA LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana ameifungia timu yake, KRC Genk katika sare ya 1-1 na Kortrijk kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Pamoja na sare hiyo, Genk inaendelea kuongoza Ligi ya Ubelgiji ikifikisha pointi 39, ikifuatiwa na Club Brugge yenye pointi 34 baada ya wote kucheza mechi 18, wakati Antwerp yenye pointi 32 za mechi 17 ni ya tatu.
  Samatta jana alifunga bao lake dakika ya 20 akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenza, Mbelgiji Leandro Trossard, kabla ya wageni kusawazisha dakika ya 45 kupitia kwa Julien De Sart aliyemalizia pasi ya Elohim Rolland.
  Mbwana Samatta (kulia) akipongezwa na wenzake baada ya kufunga jana  
  Mbwana Samatta akimuacha chini mchezaji wa Kortrijk jana Uwanja wa Luminus Arena 
  Mbwana Samatta katika mchezo wa jana Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk 

  Mbwana Samatta akimtoka mchezaji wa Kortrijk jana Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk 

  Samatta jana amecheza mechi ya 133 katika mashindano yote tangu amejiunga na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akiwa jumla ya mabao 52.
  Katika Ligi ya Ubelgiji pekee amefikisha mechi 103 na kufunga mabao 37, Kombe la Ubelgiji mechi nane na mabao mawili na Europa League mechi 22 mabao 14.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest, Uronen/B. Nastic dk77, Berge/Fiolic dk63, Malinovskyi, Pozuelo, Ndongala/Gano dk54, Trossard na Samatta.
  KV Kortrijk; Kaminski, Kumordzi, Kagelmacher, Azouni, Van Der Bruggen, Avenatti/Stojanovic dk66, De Sart, Rolland, Batsula/Hines-Ike dk89, D'Haene na Ezekiel/Chevalier dk75.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AFUNGA BAO LA KUONGOZA KRC GENK YALAZIMISHWA SARE YA 1-1 NA KORTRIJK KATIKA LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top