• HABARI MPYA

  Sunday, December 09, 2018

  CHELSEA YAICHAPA MAN CITY 2-0 NA KUIONDOA KILELENI ENGLAND

  Cezar Azpilicueta akiwa amembeba N'Golo Kante kumpongeza baada ya kuifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya 45 katkka ushindi wa 2-0 dhidi ya Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge mjini London usiku wa jana. Bao la pili lilifungwa na David Luiz dakika ya 78, pasi za mabao yote akitoa Edin Hazard na kwa matokeo hayo Manchester City ya kocha Pep Guardiola inapoteza mechi ya kwanza ya msimu.
  Man City inayobaki na pointi zake 41 baada ya kucheza mechi 16, sasa inaipisha kileleni Liverpool yenye pointi 42 za mechi 41 pia, ambayo inabaki kuwa timu pekee ambayo haijapoteza mechi hadi sasa msimu huu 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHELSEA YAICHAPA MAN CITY 2-0 NA KUIONDOA KILELENI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top