• HABARI MPYA

  Saturday, December 01, 2018

  CAF YAIVUA CAMEROON UENYEJI WA AFCON KWA MAANDALIZI DUNI

  SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeipokonya Cameroon uenyeji Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa sababu haijaridhishwa na maandalizi yao.
  Taarifa ya CAF jana imesema kwamba maamuzi hayo yamechukuliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya shirikisho hilo kilichofanyika mjini Accra, Ghana juzi.
  Maamuzi hayo ambayo hayana nafasi ya rufaa, yanamaanisha sasa CAF itafungua milango kwa mwenyeji mwingine wa mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika katikati ya mwakani.

  Sasa tiketi ya Cameroon kwenda kutetea Kombe la AFCON ipo kwa Comoro

  CAF imeahidi kumtambulisha mwenyeji mpya wa AFCON ifikapo Desemba 31, mwaka huu huku Cameroon ikipewa kipaumbele katika uenyeji wa fainali zijazo.
  Isingepokonywa uenyeji, Cameroon ingeandaa michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1972.
  Simba Wasiofungika wa Cameroon kwa sasa ndiyo mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kutwaa Kombe hilo kwa mara ya tano kihistoria katika michuano iliyopita wakiifunga Misri 2-1 katika fainali Uwanja wa L'Amitie mjini Libreville nchini Gabon.
  Na Cameroon wanakuwa wenyeji wa pili mfululizo kupokwa haki ya kuandaa michuano hiyo kwa sababu ya maandalizi duni, baada ya Kenya mwaka 2017 ambao walipokewa na Gabon.
  Sasa Cameroon watatakiwa kushinda dhidi ya Machi 22, mwakani ili kupata tiketi ya kwenda kutetea Kombe lao katika fainali zijazo.
  Kwa sasa Cameroon inashika nafasi ya pili kwenye Kundi B ikiwa na pointi nane baada ya kucheza mechi tano, ikiwa nyuma ya Morocco yenye pointi 10 za mechi tano pia, wakati Comoro ni ya tatu kwa pointi zake tano na Malawi yenye pointi nne.   
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAIVUA CAMEROON UENYEJI WA AFCON KWA MAANDALIZI DUNI Rating: 5 Reviewed By: Boaz Mwakasege

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top