• HABARI MPYA

  Sunday, November 11, 2018

  YANGA SC YAINYOOSHA AFRICAN LYON, YAICHAPA BAO 1-0 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI UWANJA WA UHURU DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, African Lyon katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Pius Charles Buswita dakika ya 42 kwa shuti kali la kitaalamu baada ya kuwatoka mabeki wa African Lyon kufuatia pasi ya beki wa kulia na Nahodha wa leo, Juma Abdul Jaffar.
  Bao hilo lilikuja baada ya Yanga SC kupoteza nafasi nyingi za wazi za kufunga kutokana na umakini mdogo wa washambuliaji wake, Buswita na Yohanna Nkomola.

  Lyon iliyoongozwa na mkongwe wake, kiungo mshambuliaji wake, Haruna Moshi ‘Boban’ nayo ilitengeneza nafasi kadhaa, lakini tatizo likawa kwenye umaliziaji.
  Kipindi cha pili pamoja na timu zote kufanya mabadiliko, lakini ubao wa matokeo uliendelea kusomema Yanga 1-0 African Lyon.     
  Kikosi cha African Lyon kilikuwa; Erick Mahilo/Tony Charles dk37, Salum Daudi, Kassim Simbaulanga, Augustino Samson/Said Mtikila dk58, Rashid Mangula/Roland Narcise dk63, Ismail Gambo, Khalfan Mbarouk, Gervas Bernard, Kassim Kilungo/Joseph Isaac dk85, Haruna Moshi ‘Boban’ na Baraka Jaffar/Malik Kapolo dk75.
  Yanga SC; Claus Kindoki, Juma Abdul, Mwinyi Mngwali, Cleophas Sospeter/Andrew Vincent ‘Dante’ dk78, Pato Ngonyani/Maka Edward dk72, Said Juma ‘Makapu’, Yussuf Mhilu/Heritier Makambo dk70, Raphael Daudi/Thabani Kamusoko dk69, Pius Buswita/Said Mussa ‘Ronaldo’ dk46, Yohanna Nkomola/Matheo Anthony dk77 na Emmanuel Martin/Jaffar Mohammed dk83.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YAINYOOSHA AFRICAN LYON, YAICHAPA BAO 1-0 KATIKA MECHI YA KIRAFIKI UWANJA WA UHURU DAR Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top