• HABARI MPYA

  Sunday, November 04, 2018

  SIMBA SC YATAKA KUTUMIA SH BILIONI 6.3 MSIMU UJAO KUJENGA TIMU YA KUTISHA ZAIDI AFRIKA NZIMA

  Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba imepanga kutumia Sh 6.3 bilioni katika bajeti yake ya kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2019.
  Wakati ikipanga kutumia bajeti hiyo, Simba itaingiza Sh 4.9 bilioni kutoka kwenye vyanzo vyake vya mapato.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyoanishwa kwenye mkutano mkuu, klabu hiyo itakuwa na hasara ya Sh 1.3 b kwenye bajeti yake ya hadi Juni mwakani.
  Katika bajeti hiyo wachezaji wa Simba wametengewa kitita cha Sh 400 Milioni kama bonasi katika msimu wa 2018/2019.
  Katika hatua nyingine, Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba imemteua aliyekuwa Mwenyekiti wa kundi la Friends of Simba, Crescentius Magori kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo baada ya kufanyika kwa uchaguzi leo.
  Kaimu Rais wa Simba SC, Salum Abdallah 'Try Again' akipiga kura
  Mwenyekiti wa zamani wa Simba SC, Hassan Daalal akipiga kura
  Mwanachama maarufu wa Simba SC, Bi Hindu akipiga kura
  Mtendaji Mkuu mpya wa Simba SC, Crescentius Magori akiwa kwenye ukumbi wa mkutano 
  Wanachama wa Simba SC wakiwa kwenye ukumbi wa mkutano leo tayari kuchagua viongozi wao wapya

  Simba leo imeweka historia ya aina yake baada ya kuingia katika mfumo mpya wa uendeshaji kufuatia mwamachama na mfanyabiashara mkubwa nchini, Mohammed 'Mo' Dewji kukubali kununua asilimia 49 ya hisa za klabu ili kuwekeza.
  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kawaida, Kaimu Rais wa Simba Salum Abdallah 'Try Again' alisema jina la Magori limeanza kazi rasmi baada ya Bodi kuanza kazi yake.
  Magori aliwashukuru wana Simba kumkubali na pia bodi ya Wakurugenzi kuona anafaa katika nafasi hiyo hivyo hawezi kuwawangusha katika Utendaji kazi wake.
  "Mimi mnanijua vizuri tu, kwanza niwaambie baada ya kuambiwa nafasi hii nilitafakari sana, lakini kwa mapenzi ya Simba sikuwa na shaka. Nina imani tutafanya kazi vizuri," alisema.
  Adha Magori aliwataka wanachama kuhakikisha wanampa ushirikiano mkubwa katika utendaji kazi wake ili Simba ifike mbali zaidi ya hapa.
  Katika hotuba yake akiwa Kaimu amejivunia kuondoa migogoro mikibwa iliyokuwepo ndani mpaka kupelekea simba inafanya vizuri 
  "Wakati naingia nillkuta migogoro mikubwa ila. Najivunia kuiondoa, kwa sasa kila mtu anafanya kazi yake na hata wachezaji wanafanya majukumu yao,"akisema.
  Alisema wanaimani kubwa mpaka Oktoba mwakani uwanja wa Bunju uwe umetimia ili kupunguza gharama kubwa.
  Aidha Try alilishukuru uongozi wa aliyewahi kuwa Mwenyekiti hapo zamani Hassan Dalali kwa hatua zake na wenzake katika upatikanaji wa uwanja huo.
  Aliwataka wanachama kuacha mihemko na kuchagua viongozi ambao wataingia kuisaidia Simba na sii Simba ikawasaidiae wao.
  "Najua wanachama wagombea unawajua uchaguen watu mazuri wenye uwezo mkubwa wa kwenda kujenga hoja na sio kuwa nasikiliza,"akisema huku wanasimba zaidi ya 1480 walimshangilia.
  Alisema anajivunia pia kusajili nyota 10 wakali kutoka Twiga Stars, ili kuboresha kkko hicho.
  Alisema timu ya wanawake iko vizuri kwa ajili ya kukabiliana na timu yoyote ile. Hivyo viongizi wajao wakaendekeze.
  Aidha Try alisema licha ya kumaliza muda wake atahakikisha anashirikiana na watakaochaguliwa kuiendesha timu hiyo.
  Kuhusu madeni try alisema walikuta madeni mengi na wameyalipa huku kwa upande wa kodi wakidaiwa mil 800 ambapo wamejitahidi kuripa kwa kutambua kodi wajibu.
  Majira ya saa 5 Mzee Hamis Kilomon aliingia ukumbini huku akishangiliwa na wanachama na kupewa kiti mbele wakikoketi viongozi mbalimbali wakiwemo Abdallah Burembo, Adam Mgoi, Juma Kapuya, Hassanoo na wengineo.
  Kwa kutambua kauli mbiu ya Simba nguvu moja wanachama hao wamesamehewa ili kuwa kitu kimoja na kutakuwa kuondoa mashtka yao katika mahakama.
  Alisema makundi yaondolewe ili iwe nguvu moja na kitu kimoja.
  Awali ya hapo, Mgombea ujumbe Mwina Kaduguda aliibua gumzo baada ya kupanda meza ya viongozi kwa kudai hana imani na akidi ya watu 1728 iliyotangazwa akidai siyo kweli huku akiitaka kamati ya uchaguzi kuhesabu watu upya.
  Awali ilitangazwa jumla ya wanachama 1486 na baadae wakaongezeka hadi kufikia 1728 kitendo hicho kulimfanya Kaduguda kupanda juu na Polisi kulazimika kumtoa nje kwa muda wa dakika 15 na baadaye kumrejesha huku akikumbatiana na viongozi kuashiria kukubali matokeo.
  Wanachama walimshangaa kaduguda na kuhoji uwezo wake endapo atachaguliwa huku wachache walimshangilia.
  Aidha, baada ya sintofahamu hiyo Mwenyekiti alipigwa butwaa baada ya kuona malalamiko hayo huku aliwataka wanachama kuwa watulivu ili uchaguzi ufanyike kwa amani.
  "Nashangaa sana kuona hii, kwani akidi wakati natangaza 1720 na kuongezeka wanachama wanane, sasa nashangaa tatizo nini,"alisema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YATAKA KUTUMIA SH BILIONI 6.3 MSIMU UJAO KUJENGA TIMU YA KUTISHA ZAIDI AFRIKA NZIMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top