• HABARI MPYA

  Sunday, November 04, 2018

  NGOMA AIFUNGIA BAO PEKEE AZAM YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR LAKINI ALIMWA KADI NYEKUNDU DAKIKA YA MWISHO

  Na Mwandishi Wetu, BUKOBA
  AZAM FC imendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Kagera Sugar 1-0 mchana wa leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
  Ushindi huo umetokana na bao pekee la mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Dombo Ngoma aliye katika msimu wake wa kwanza tangu asajiliwe kutoka Yanga SC aliyefunga dakika ya 40, kabla ya kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 90 na ushei.
  Na sasa timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inafikisha pointi 30 baada ya kucheza mechi 12, ikiendelea kuongoza Ligi Kuu.

  Azam FC inayofundishwa na kocha Mholanzi, Hans van der Pluijm inafuatiwa na mabingwa watetezi, Simba SC wenye pointi 26 za mechi 11, wakati Yanga ambayo usiku wa leo itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC ipo nafasi ya tatu kwa pointi zake 25 za mechi tisa.
  Mbali na Yanga SC na Ndanda FC Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Saa 1:00 usiku, mechi mbili ya Ligi Kuu leo ni kati ya Mwadui FC na Tanzania Prisons Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga iliyoanza Saa 10:00 jioni hii.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGOMA AIFUNGIA BAO PEKEE AZAM YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR LAKINI ALIMWA KADI NYEKUNDU DAKIKA YA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top