• HABARI MPYA

  Friday, November 09, 2018

  SIMBA SC YAPEWA VIBONDE WA SWAZILAND, WAKIWATOA WATAKUTANA NA SONGO AU AKINA HASSAN KESSY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba ya Dar es Salaam itaanza na Mbabane Swallows Swaziland katika Raundi ya Awali ya mchujo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2019.
  Ikifanikiwa kuvuka mtihani huo, Simba SC itakwenda hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo.
  Na huko itamenyana na mshindi kati ya Uniao Desportiva Do Songo ya Msumbiji na Nkana FC ya Zambia, anayochezea beki wake wa zamani, Mtanzania, Hassan Kessy aliyewahi kucheza na Yanga pia.
  Wawakilishi wa Zanzibar, JKU watamenyana na Al Hilal ya Sudan na mshindi baina yao atakutanana mshindi kati ya APR FC ya Rwanda na Club Africain ya Tunisia.

  Mechi za kwanza za raundi ya kwanza ya mchujo zitachezwa kati ya Novemba 27 na 28 na marudiano Desemba 4 na 5, mwaka huu, wakati mechi za kwanza za raundi ya pili ya pili na ya mwisho ya mchujo zitachezwa kati ya Desemba 14 na 16 na marudiano Desemba 21 na 23, mwaka huu.
  Katika Kombe la Shirikisho, Mtibwa Sugar itaanza na Northern Dynamo ya Shelisheli na ikivuka mtihani huo itakutana na K.C.C.A ya Uganda.
  Wawakilishi wa Zanzibar, Zimamoto wamepewa kigongo, Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini na mshindi baina yao atakutana na mshindi kati ya El Geco ya Madagascar na Deportivo Unidad ya Equatorial Guinea.
  GONGA HAPA KUTAZAMA RATIBA KAMILI LIGI YA MABINGWA 
  GONGA HAPA KUTAZAMA RATIBA KAMILI KOMBE LA SHIRIKISHO
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAPEWA VIBONDE WA SWAZILAND, WAKIWATOA WATAKUTANA NA SONGO AU AKINA HASSAN KESSY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top