• HABARI MPYA

  Friday, November 09, 2018

  RAHIM MUNISI WA YOMBO VITUKA AINGIA KWENYE ORODHA YA WASHINDI WA BAJAJI ZA SPORTPESA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMPUNI ya michezo ya kubashiri SportPesa inaendelea kubadili maisha ya watanzania kwa kutoa zawadi mbalimbali kupitia promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa. Promosheni hii inawawezesha watanzania kutoka mikoa yote kujishindia zawadi kama Bajaji, Jezi ya Simba na Yanga, simu za mkononi (Smartohones pamoja na tiketi za kuhudhuria mechi za ligi kuu inayoendelea nchini Hispania na Uingereza).
  Kupitia *150*87# na kuweka pesa kwenye akaunti yako kuanzia shilingi 1000 kutapelekea mtumiaji wa mitandao yote ya simu kui ngia kwenye droo kujishindia zawadi hizo mara baada ya kuweka ubashiri wake kila siku.

  Akishuhudia ushindi wake mkazi wa Yombo Vituka kwa masizi hapa jijini Dar es Salaam, ambapo hapo  mshindi wa droo ya 44 katika shinda zaidi na sportpesa huyu ni Rahim Munisi yuko tayari kukabidhiwa bajaj yake ya ushindi.
  Akiwa mwenye furaha munisi aliipokea timu ya ushindi akiwa na jamaa ndugu pamoja rafiki zake ambao wote walikuwa mashuhuda wakati anakabidhiwa bajaj.
  Akizungumza machache mara baada ya kuchukua chombo chake cha ushindi Munisi alisema kuwa alianza kucheza na sportpesa baada ya kuona kipindi cha shinda zaidi kwenye televisheni sambamba na matangazo yanayoruka kwenye mitandao ya kijamii ya sportpesa.
  "Nimeshinda kweli siamini mimi nilikuwa dereva bodaboda kitendo cha kushinda bajaj hii kutoka sportpesa ni kama niko ndotoni lakini kumbe ndio ukweli aisee na ndio mnanikabidhi hivi sasa kwangu hii ni hatua kutoka kwenye bodaboda mpaka bajaj nimeshatusua mwenzenu yani sportpesa nyie ni watu wema sana " alisema Munisi.
  Mshindi huyo alisema kipato kitakachotokana na bajaj hiyo kitamsaidia sana hasa kwenye kuboresha maisha ya familia ikiwa ni pamoja na kumuwezesha kusomesha watoto wake vyema kwani kupata ada ilikuwa mtihani mkubwa kwake 
  Ilikuwa shangwe sana kwenye viunga vya mtaa wa yombo maana wananchi na majirani zake munisi waliufurahia ushindi huo na mara zote walisikika wakiimba tumeshinda!!tumeshinda!! tumeshinda!!!
  Kutoka SportPesa Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti SportPesa Tanzania Tarimba Abbas alisema “ Tunakaribiri kufikia nusu ya promosheni hii ambapo mpaka sasa tumepata washindi 49 kutoka mikoa mbalimbali nchini, Watanzania wakati ni huu kuchangamkia nafasi hii ili kubadili maisha yako”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAHIM MUNISI WA YOMBO VITUKA AINGIA KWENYE ORODHA YA WASHINDI WA BAJAJI ZA SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top