• HABARI MPYA

  Friday, November 02, 2018

  SERIKALI YAAGIZA YANGA SC KUFANYA UCHAGUZI ILI KUPATA SAFU MPYA YA UONGOZI IMARA BAADA YA WENGI KUJIUZULU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limeiagiza klabu ya Yanga kuitisha uchaguzi wa kujaza nafasi za viongozi waliojiuzulu ili kuwa na safu imara ya uongozi.
  Taarifa ya BMT kwa vyombo vya Habari imesema kwamba, Yanga imebaki na Wajumbe sita kati ya 13 waliochaguliwa katika uchaguzi wa Juni 12, mwaka 2016 Dar es Salaam.
  “Kwa mantiki hiyo, klabu ya Yanga inatakiwa kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi zilizo wazi katika uongozi kwa mujibu wa katiba yao wenyewe,”imesema taarifa ya BMT.
  Na hiyo ni baada ya vikao vilivyohusisha Wazee, Wanachama, Viongozi na wadau mbalimbali wa klabu hiyo vilivyohudhuriwa hadi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.

  BMT imesema kwamba uchaguzi huo utasimamiwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na mapungufu ya Akidi katika Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo.
  Na kuhusu mkanganyiko wa kadi za uanachama, BMT imeagiza lifanyike zoezi la kusajili wanachama wenye kadi za zamani ili kurejesha umoja na mshikamano ndani ya klabu.  
  Yanga SC imebaki na Wajumbe sita tu baada ya viongozi wote wakuu kujiuzulu kwa wakati tofauti, akiwmeo Mwenyekiti, Yussuf Manji na Makamu wake, Clement Sanga.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERIKALI YAAGIZA YANGA SC KUFANYA UCHAGUZI ILI KUPATA SAFU MPYA YA UONGOZI IMARA BAADA YA WENGI KUJIUZULU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top