• HABARI MPYA

    Monday, November 12, 2018

    SAMATTA AFIKISHA MECHI 100 LIGI YA UBELGIJI GENK IKIENDELEZA REKODI YA KUTOFUNGWA MSIMU HUU

    Na Mwandishi Wetu, MOUSCRON
    MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefikisha mechi 100 za kucheza Ligi Daraja la Kwanza Ubelgiji, maarufu kama Belgian Pro League, timu yake, KRC Genk ikiendeleza rekodi yaa kutopoteza mechi msimu huu baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Royal Excel Mouscron usiku wa jana Uwanja wa Le Canonnier mjini Mouscron.
    Samatta alicheza kwa bidii jana akipambana na mabeki hodari wa Royal Excel Mouscron walioongozwa na Msenegal, Christophe Diedhiou lakini akashindwa kufunga tu. 
    Mbwana Samatta akimtoka beki wa Royal Excel Mouscron usiku wa jana Uwanja wa Le Canonnier mjini Mouscron 
    Mbwana Samatta akipambana na beki Msenegal wa Royal Excel Mouscron jana, Christophe Diedhiou

    Kwa matokeo hayo, Genk inaendelea kuongoza ligi ya Ubelgiji ikifikisha pointi 35 baada ya kutoa sare ya tano jana katika mechi 15 ilizocheza, nyingine zote 10 ikishinda. Inafuatiwa na Club Brugge yenye pointi 31 za mechi 15 pia na sawa na Antwerp. 
    Kwa ujumla Samatta jana amefikisha mechi 129 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 51.
    Katika Ligi ya Ubelgiji pekee amefikisha mechi 100 na kufunga mabao 36, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 21 mabao 14.
    Kikosi cha Mouscron jana kilikuwa; Butez, Dussenne, Olinga/Kuzmanovic dk75, Mohamed, Gkalitsios, Boya, Sarmiento/Kalonji dk72, Pierrot, Diedhiou/Mbombo dk95, Chibani na Godeau.
    KRC Genk; Vukovic, Maehle, Aidoo, Dewaest, Nastic/Uron dk45, Berge, Malinovskyi, Pozuelo, Zhegrova/Trossard dk62, Ndongala/Heynen dk79 na Samatta.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA AFIKISHA MECHI 100 LIGI YA UBELGIJI GENK IKIENDELEZA REKODI YA KUTOFUNGWA MSIMU HUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top