• HABARI MPYA

  Tuesday, November 06, 2018

  SALEH LIBENANGA: KIPA ANAYETAKA KUIREJESHA NJOMBE MJI LIGI KUU KABLA YA KWENDA KUKIPIGA ULAYA

  Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
  KATIKA maisha kila mtu anakuwa na malengo yake hasa na kile kitu anachokifanya ili aweze kufika mbali kimaisha.
  Kuna changamoto nyingi wanapitia ili kuweza kukwama lakini kutokana na uimara na kujiamini unajikuta unafika mbali na kuwashangaza wale ambao walikuwa hawataki maendeleo yako.
  Kila mmoja anapenda kuhakikisha anafanikisha lile ambalo amelikusudia ndio maana wengi wao hufanya kazi kwa bidii na kubadili maisha yao.
  Leo tutakuwa na kipa wa Njombe Mji, Saleh Libenanga, ambaye atatuelezea mambo mengi kuhusu maisha ya mpira na pia jinsi gani alivyohuzunika pindi timu yake iliposhuka daraja.

  Saleh Libenanga, kipa namba moja wa timu ya Njombe Mji FC inayopigana kurejea Ligi Kuu

  SWALI: Mambo Libenanga.
  JIBU: Salama.
  SWALI: Ilikuwaje ukajiingiza kwenye masuala ya mpira na siyo fani nyingine yeyote ambayo unaona ingekuingizia kipato zaidi?
  JIBU: Kikukweli mimi nilivyozalia nilikuwa najiona kabisa kama nina kipaji cha mpira na ndio maana tangu utoto hadi nikiwa shuleni nilikuwa nashiriki sana kwenye soka.
  SWALI: Ilikuwaje ukawa unacheza nafasi ya kipa na si nafasi nyingine yeyote?
  JIBU: Kila nilipokuwa nacheza mpira na wezangu walikuwa wananifanya mimi kuwa golikipa na nafasi hiyo nikawa naimudu zaidi kuliko nafasi nyingine yeyote na ndio nikawa nimezoea hadi leo.
  SWALI: Ni mchezaji gani ambaye alikuwa anakuvutia zaidi na mara nyingine huwa unacheza kama yeye.
  JIBU: Kiukweli tangu naanza kucheza mpira nilikuwa napenda sana kumuangalia golikipa wa KM C, Juma Kaseja na kuna vitu vingi sana najifunza kutoka kwake na naamini siku moja na mimi nitakuwa kama yeye 'Tanzania One'.
  Lakini kwa sasa napenda sana kumuangalia golikipa wa Mtibwa, Shabani Kado sababu amekua na vitu vingi bora ambavyo akiwa kwenye mechi huwa namtazama kwa umakini.
  SWALI:Ukiacha nafasi unayocheza je ukiwa uwanjani ni nafasi gani nyingine ukipangwa unaimudu vizuri?
  JIBU: Ukiacha nafasi hii niliyopo sasa kama mwalimu akiamua kunipanga nafasi nyingine huwa naweza kucheza nafasi ya ushambuliaji au kiungo.
  Lakini kama nikiwa mapumziko nyumbani Morogoro, tunakuwa na timu yetu ya Magolikipa inaitwa Features Goalkeeper's, huwa tunacheza mechi na mara nyingi huwa napangwa kama mshambuliaji na huwa nafunga magoli mengi tu.
  SWALI: Siku timu yako ya Njombe Mji ilipopanda daraja ulijiskiaje kama wewe ukiwa mmoja wa wachezaji wa timu hiyo.
  JIBU:  Kiukweli nilifurahi sana kwakweli sababu nilijua nikiingia kwenye Ligi Kuu nitaonesha kipaji changu  na kuona kuwa ndoto zangu zingetimia kwa hatua ambayo nilikuwa nimefikia.
  SWALI: Na je iliposhuka daraja hali ilikuwaje?
  JIBU: Kiukweli nilijiskia vibaya sana, niliumia moyoni mwangu sababu kama wachezaji tulitumia nguvu kubwa kuhakikisha tunaipandisha daraja na leo imeshuka basi ikawa imenipotezea ndoto zangu nyingi za kufika mbali kwenye soka.
  Lakini sikukata tamaa naamini mungu kuna kitu alikuwa anakipanga na sasa nimekuwa mchezaji ambaye nafanya kazi kubwa na kwa bidii kuhakikisha timu yetu inarudi Ligi Kuu.
  SWALI: Hadi kufikia hapo ulipo unatamani kuchezea timu gani kubwa ya Ligi kuu.
  JIBU: Mimi natamani kuchezea klabu yeyote kubwa kama Simba, Yanga, Azam sababu najua nikipata nafasi kwenye timu hizo kipaji changu kitakuwa zaidi na malengo yagu yataongezeka.
  Ila siyo kama timu zingine zinazoshiriki ligi kuu zikiinitaji nikataae hapana mimi naangalia maslahi ya timu na kokote naweza kutumikia.
  SWALI: Ni jambo gani baya ambalo kila ukilikumbuka lazima utokwe machozi na hata kama unafuraha huwa inakata mara moja.
  JIBU: Siku ambayo nimempoteza mama yangu mzazi sitakuja kusahau na mara nyingine kikikumbuka maneno yake huwa napoteza furaha hata kama ninafuraha kwa kipindi hicho.
  SWALI: Je ukiacha mpira unapenda kusikiliza muziki na muziki wa mwanamuziki gani?
  JIBU: Mimi huwa napenda sana muziki na mara nyingi huwa napenda kumsikiliza  Abedinego Damian, ‘Belle 9’, kuliko mwanamuziki yeyote wa Bongo.
  SWALI:Unamalengo gani kwenye soka baada ya miaka mitano ijayo.
  JIBU: Kwanza kuisaidia timu yangu iweze kupanda daraja kwa mara nyingine lakini pia kuja kucheza soka la kulipwa hapo baadae.
  SWALI: Je ukipata nafasi ya kukutana na  raisi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia utamshauri nini kwa ajili ya kuendeleza soka la Tanzania.
  JIBU: Kwanza kabisa nitamshauri awekeze sana kwenye soka la vijana sababu kuna vipaji vingi lakini havina msaada, lakini pia ahakikishe Ligi ziwe na wadhamini kuanzia Ligi Kuu, Ligi Daraja la kwanza na Ligi Daraja la pili sababu italeta motisha kwa wachezaji sababu wanajipatia kipato.
  SWALI: Kwenye ligi daraja la kwanza kunakuwa na changamoto nyingi sana je kama wachezaji huwa mnakabiliana nazo vipi?
  JIBU: Tunajitahidi kukabiliana na changamoto zote sababu ligi ya huku ni ngumu, hakuna hela timu huwa zinakamiana na vurugu huwa nyingi lakini sababu kuna  kitu unakitaka inabidi kukabiliana nazo ili kufanikisha malengo.
  SWALI: Kwa mwenendo mnaokwenda nao Njombe Mji kwenye ligi daraja la kwanza mnadhani kama wachezaji mnaweza kuipandisha tena timu?
  JIBU: Uwezekano wa kupanda ligi kuu upo kwa asilimia kubwa sana kama wachezaji tunapambana kuhakikisha tunashinda na kurudi tena kwenye ligi sababu mechi bado nyingi na tutapambana tushinde kila mechi.
  SWALI: Ebu tuelezee kiufupi historia yako tangu ulipoanza kujiingiza kwenye mpira hadi kufikia hapa ulipo.
  JIBU: Mpira nilianza tangu nilipokuwa mdogo kipindi hicho timu yetu ya mtaani ilikuwa inaitwa Botafogo, baada ya hapo nikatoka nikaenda kucheza Moro Kids Accademy huku pia nilikuwa nacheza kwenye timu ya shule.

  Saleh Libenanga (kushoto) akiwa na kipa mkongwe, Shaaban Kado wa Mtibwa Sugar  

  Baada ya hapo nilikuwa kwenye timu ya mkoa ya Copa cocacola 2011 hado 2012 baada ya hapo 2012-2013 nilicheza nilicheza Polisi Moro timu B, baada ya hapo nikatoa nikaenda timu ya Sabasaba ya moro ambayo ilikuwa inashiriki ligi daraja la pili baada ya hapo sasa ndo nikasajiliwa na Njombe Mji na nikaisaidia timu yangu ikapanda ligi kuu ndo ndo hiyo nipo nayo hadi sasa na muomba Mungu tufanye juhudi ili kuweza kuipandisha tena. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SALEH LIBENANGA: KIPA ANAYETAKA KUIREJESHA NJOMBE MJI LIGI KUU KABLA YA KWENDA KUKIPIGA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top