• HABARI MPYA

  Tuesday, November 06, 2018

  ABDULHALIM HUMUD 'AFUKUZWA' KMC KWA SABABU YA KUTONGOZA WAKE NA MAHAWARA WA WACHEZAJI WAKE

  Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
  UONGOZI wa Klabu ya KMC umetangaza kuachana rasmi na kiungo wake, Abdulhalim Humud 'Gaucho' kufuatia malalamiko ya kudaiwa kutaka kutembea na wake pamoja na mahawara wa wachezaji wenzake.
  Humud alipeleka barua ya kutaka kuachana na timu hiyo iliyopanda daraja kushiriki Ligi Kuu msimu, kabla ya uongozi kutangaza kuachana naye.  
  Akizungumza na Waandishi wa habari leo mjini Dar es Salaam, Meneja wa KMC, Walter Harrison amesema kwamba Humud aliwasilisha barua hiyo ikiwa ni muda mfupi kupita tangu asimamishwe kuitumikia timu hiyo kutokana na makosa ya kinidhamu.

  Abdulhalim Humud 'Gaucho' ameondolewa KMC kwa makosa ya kutongoza na wake na wapenzi wa wachezaji wenzake 

  Makosa hayo ni pamoja kuacha vifaa vya michezo jijini Dar es Salaam wakati KMC ikienda kucheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union mjini Tanga, lakini pia kuwasumbua wake na wapenzi wa wachezaji wenzake ndani ya nje ya KMC.

  Harrison amesema kwamba uongozi ulipopata malalamiko hayo, ukazungumza na mchezaji mwenyewe, akakiri kufanya kosa na akaomba radhi, hivyo kusimamishwa katika timu. Amesema lakini kabla ya kupewa tamko jingine, Humud akatuma barua ya kuomba kuachana na timu na mwalimu akapitisha uamuzi wa mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa.
  "Tulipata malalamiko ya wachezaji hao na baada ya kupata ushahidi, mwalimu alimsimamisha na kabla ya adhabu kwisha Humud akatuma barua ya kuomba kuachwa na timu,"amesema Harrison.
  Humud ambaye hapo awali aliwahi kuzitumikia Simba SC, Coastal Union na Azam FC, alijiunga na KMC mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ABDULHALIM HUMUD 'AFUKUZWA' KMC KWA SABABU YA KUTONGOZA WAKE NA MAHAWARA WA WACHEZAJI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top