• HABARI MPYA

  Sunday, November 04, 2018

  MUSSA MATHIAS WA DAR ASIMULIA ALIVYOANZA KUCHEZA HADI KUWA MSHINDI WA DROO YA 34 YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA

  UNAWEZA kusema watanzania wameamua na kila mtu anapambana kwa nafasi yake kuhakikisha anashinda na timu ya ushindi SportPesa Hii ni kutokana na ubashiri na haya yote ni kujitahidi kushinda bajaj na kufungua ukurasa mpya.
  Kwanini watanzania wameamua kuipa jina la timu ya ushindi SportPesa kikubwa ni namna ambavyo timu hii imeonyesha kuwajali maana kwenye promosheni ya Shinda zaidi Na SportPesa wanatoa bajaj mia na Mtanzania mmoja anaondoka na bajaj yake kila siku hii ndio maana halisi ya timu ya ushindi yani hawakubali ubashiri wako ukuache hivi hivi.
  Na kama kawaida SportPesa imeendelea kutoa bajaj kwa washindi wa promosheni ya shinda zaidi huku kwa wakati huu Mussa Mathias Kutoka Hapa Jijini Dar es salaam ndiye anayekabidhiwa bajaj baada ya kushinda.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas(kushoto) akimkabidhi funguo za bajaji Mussa Mathias mjini Dar es Salaam 

  Huyu ni mshindi wa droo ya 34 ambaye alitusimulia ni kwa vipi alianza kucheza na timu ya ushindi mpaka kufanikiwa kushinda bajaj na hatimaye kuanza mwanzo mpya katika Maisha.
  Mathias alisema watu wa huduma kwa wateja kutoka SportPesa ndio walimsababisha kujiunga na kuanza kucheza na hii ilitokea siku ambayo walikuwa wanapita mtaani kutoa elimu kuhusu timu ya ushindi ndipo na yeye alishawishika na kuanza kucheza.
  "kwenye maisha kuna mambo mengi sana mimi ni dereva bajaj nimepitia mambo mengi nilikuwa natamani siku moja kumiliki bajaj yangu mpya ila sikufahamu ni wapi pangekamilisha ndoto yangu hii, ndio maana nilivyosikia na nyie mnatoa bajaj nilijitajidi kucheza sana kweli mungu sio dhalimu na mimi nimebahatika kushinda kweli hata siamini ila ama hakika sportpesa mmekwamua maisha yangu nawashukuru sana " alisema Mathias.
  Hata hivyo mshindi huyo anaamini kupitia bajaj hiyo ni mwanzo wa yeye kuanza maisha mapya ya ushindi huku akiwa na ndoto ya kujenga nyumba kubwa kutokana na kipato atakachoingiza sambamba na kuishi maisha bora yeye na familia yake.
  Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti kutoka SportPesa Tarimba Abbas alimpongeza mshindi huyo wakati akimkabidhi bajaj na kumtaka kuitumia vyema na kuifanya kuwa chanzo chake kikubwa kumuingizia kipato.
  "Hongera sana kwa kushinda hii imekuwa bahati yako na kama ukiweka mikakati mizuri basi bajaj hii itakuingizia kipato kikubwa sana sisi kama sportpesa tunakupongeza usiache kucheza maana bado kuna vitu vingi vya kushinda" alisema Tarimba.
  Mwisho kabisa aliwasisitiza watanzania kuendelea kucheza na SportPesa akidai kuwa mbali ya kushinda bajaj unaweza kushinda tiketi ya kushuhudia mechi za ligi kuu uingereza na spain huku zawadi nyingine ikiwa ni simu janja smartphone na jezi original za Simba Na Yanga
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MUSSA MATHIAS WA DAR ASIMULIA ALIVYOANZA KUCHEZA HADI KUWA MSHINDI WA DROO YA 34 YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top