• HABARI MPYA

  Saturday, November 10, 2018

  MTIBWA SUGAR YASEMA HAITAWADHARAU WAPINZANI WAO WA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA KUTOKA SHELISHELI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imesema kwamba hautawadharau wapinzani wao wa kwanza katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Nothern Dynamos ya Shelisheli.
  Akizungumza mjini Dar es Salaam, Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila amesema kwamba hawawadharau wapinzani wao hao kwa sababu ni wawakilishi wao nchi yao kama wao.
  Katwila amesema timu inaposhinda nafasi ya kuiwakilisha nchi yake katika mashindano ya Afrika haiwezi kuwa ya kubezwa kwa sababu imeshindana kupata nafasi.

  Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila (kulia) amesema kwamba hawawadharau Nothern Dynamos

  "Sisi tunashukuru tumepata ratiba hii mapema na mara moja tunaanza kujipanga kwa ajili ya mtihani uliopo mbele yetu. Hatuwezi kuwadharau wapinzani wetu kisa wanatoka Shelisheli, tutajipanga kukabiliana nao," amesema Katwila ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo.
  Kwa mujibu wa ratiba iliyotoka jana, Mtibwa Sugar wataanzia nyumbani dhidi ya Nothern Dynamos Novemba 27 au 28 kabla ya kusafiri kwenda Shelisheli kwa mchezo wa marudiano kati ya Desemba 4 au 5.
  Na Iwapo 'Wana Tam Tam' watafanikiwa kuvuka hatua ya awali kwa kuwatoa Nothern Dynamos, watavaana na KCCA  ya Uganda katika hatua ya pili ya mchujo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YASEMA HAITAWADHARAU WAPINZANI WAO WA KWANZA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA KUTOKA SHELISHELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top