• HABARI MPYA

  Saturday, November 10, 2018

  MWENYEKITI WA UCHAGUZI TFF AWAONYA WANA YANGA WANAOTAKA KUTIBUA UCHAGUZI WATAKIONA CHA MOTO NA WATAJUTA

  Na Mwandishi Wetu, DODOMA
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limewaonya vikali viongozi na mashabiki wa klabu ya Yanga wanaopanga kuvuruga mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo.
  Yanga wanatarajiwa kufanya uchaguzi wake Januari 13, mwakani kwa ajili ya kuziba nafasi zilizokuwa wazi.
  Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela, alisema TFF haitowavumilia wote watakaothubutu kuvuruga mchakato huo.
  Mchungahela alisema kuwa wamebaini kwamba  kuna mkakati wa baadhi ya viongozi wa kamati ya utendaji na mashabiki wa kutaka  kuitisha mkutano kesho  wenye lengo la kupinga uchaguzi.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Malangwe Mchungahela amesema TFF haitowavumilia  wanataka kuvuruga uchaguzi wa Yanga

  “Taarifa zao tunazo, kwamba wanataka kuitisha kikao cha kupinga uchaguzi, hivyo sisi kama TFF tunawaonya wasithubutu, kwani tutawashughulikia kwa kutaka kuharibu mchakato huo na  pia yeyote yule anayetaka uongozi asipite mlango wa nyuma, tukibaini hilo basi  tutawashughulikia ikiwemo kuwapeleka kwenye kamati ya maadili,"amesema Mchungahela.
  Mchungahela alisema kuwa  awali walishakutana na viongozi waliobakia kwenye timu hiyo ambapo waliridhia kuendelea na mchakato wa uchaguzi hivyo kwa wanaotka kuharibu wanajitafutia matatizo.
  Aidha Mchungahela alisema kuwa tayari fomu za uchaguzi zimeshaanza kutolewa tangu jana  na mwisho wa kuchukua fomu hizo ni Desemba 14 mwaka huu.
  Mbali na Manji viongozi wengine wa Yanga waliojiondoa ni Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji Hashim Abdala, Salum Mkemi na Omar Said.
  Kufuatia hatua hiyo, Novemba mbili mwaka huu, Baraza la Michezo Taifa (BMT) kupitia kwa Kaimu Katibu Mkuu, Alex Kayenge iliitaka Yanga kufanya uchaguzi na kuitaka Kamati ya Uchaguzi ya TFF kusimamia uchaguzi huo ikiwemo bayana nafasi zinazopaswa kugombewa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MWENYEKITI WA UCHAGUZI TFF AWAONYA WANA YANGA WANAOTAKA KUTIBUA UCHAGUZI WATAKIONA CHA MOTO NA WATAJUTA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top