• HABARI MPYA

  Sunday, November 04, 2018

  MCHEZAJI MPYA RASTA AINUSURU YANGA KUPIGWA NYUMBANI NA NDANDA FC, WATOA SARE 1-1 UWANJA WA TAIFA

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepinguzwa kasi baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Sare hiyo inaiongezea pointi moja Yanga SC ikicheza mechi ya 10 na kufikisha pointi 26, sawa na mabingwa watetezi, Simba SC waliocheza mechi 11 ambao wanaendelea kukamata nafasi ya pili kwa wastani wao mzuri wa mabao.   
  Vigogo hao wote wapo nyuma ya Azam FC, yenye pointi 30 baada ya kucheza mechi 12 kufuatia na leo kupata ushindi wa ugenini wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.  Mchezaji mpya, Jaffar Mohammed akikimbia kushangilia baada ya kuifungia Yanga bao la kusawazisha katika sare ya 1-1 na Ndanda FC

  Katika mchezo wa leo, Ndanda walitangulia kupata bao mapema tu dakika ya 16 kupitia kwa Nassor Hashim aliyefumua shuti baada ya kupitia mpira miguuni mwa mshambuliaji mwenzake wa Ndanda FC, Vitalis Mayanga aliyempindua beki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’.
  Na hiyo ilifuatia Ndanda FC inayofundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Zanzibar, Malale Hamsini kufanya shambulizi la haraka la kushitukiza wakitoka kushambuliwa wao.  
  Hata hivyo, iliwachukua Yanga SC dakika nane tu kusawazisha bao hilo, baada ya mchezaji wake mpya, Jaffar Mohammed mweye rasta kichwani iliyemsajili kutoka Maji Maji ya Songea iliyoteremka daraja kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo mwenzake, Ibrahim Ajib dakika ya 24.
  Timu hizo zilikwenda kupunzika zikiwa zimefungana 1-1 na kipindi cha pili, Ndanda walirejea na mpango wa kucheza kwa kujihami hadi kufanikiwa kupata sare ya ugenini.  
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Beno Kakolanya, Juma Abdul/Raphael Daudi dk80, Gardiel Michael, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Andrew Vincent ‘Dante’, Feisal Salum, Mrisho Ngassa/Deus Kaseke dk70, Maka Edward, Heritier Makambo, Ibrahim Ajib na Jaffar Mohammed/Amissi Tambwe dk63.
  Ndanda FC; Diel Makonga, Aziz Sibo, Yassin Mustafa, Malika Ndeule, Rajab Rashid, Baraka Majogoro, Rajab Milandu, Muhsin Mohammed, Vitalis Mayanga, Nassor Hashim na Ahmed Msumi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MCHEZAJI MPYA RASTA AINUSURU YANGA KUPIGWA NYUMBANI NA NDANDA FC, WATOA SARE 1-1 UWANJA WA TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top