• HABARI MPYA

  Monday, November 05, 2018

  KMC YAONYESHA SI TIMU YA KUBEZA, YAIPIGA MBEYA CITY 1-0 DAR NA KUJIWEKA SAWA KATIKA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya KMC ya Kinondoni leo imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, Cliff Anthony Buyoya dakika ya 84 aliyemalizia mpira uliotemwa na kipa Owen Chaima baada ya shuti la Emmanuel Mvuyekure aliyeunganisha krosi ya Ally Msengi.
  Na sasa KMC, timu inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inafikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi 13, ingawa inabaki nafasi ya 10 katika Ligi ya timu 20, nyuma ya Singida United yenye pointi 17 za mechi 13 na mbele ya Kagera Sugar yenye pointi 16 za mechi 12. 

  Mechi ya leo, ilikutanisha makocha wa Burundi watupu, Ramadhani Nswazurimo wa Mbeya City na Etienne Ndayiragijje wa KMC  iliyopanda Ligi Kuu simu huu.
  Nswazurimo yupo katika msimu wa pili Mbeya City, wakati Ndayiragijje amejiunga na KMC msimu huu baada ya misimu miwili ya kuwa na Mbao FC ya Mwanza. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KMC YAONYESHA SI TIMU YA KUBEZA, YAIPIGA MBEYA CITY 1-0 DAR NA KUJIWEKA SAWA KATIKA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top