• HABARI MPYA

  Tuesday, November 06, 2018

  PANGANI YATOA TENA MSHINDI PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA, SAFARI HII NI MASOUD YUSUPH AJINYAKULIA BAJAJI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BAADA ya mshindi wa droo ya kwanza ya shinda zaidi na SportPesa kutokea Pangani, droo ya 34 pia imetoa mshindi toka eneo hilo. 
  Masoud Yusuph (29) hatimaye amekabidhiwa bajaj yake baada ya kushida katika promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa ambapo zawadi mbalimbali hutolewa mara baada ya mchezaji au shabiki wa michezo akiweka ubashiri wake mara baada ya kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa anapata nafasi ya kushinda zawadi kama simu za mkononi, Jersey za timu ya Simba au Yanga, tiketi ya kwenda kushuhudia mitanange ya ligi kuu nchini Uingereza na Hispania wakati Bajaji ikiwa ni zawadi kuu.
  Masoud Yusuph baada ya kukabidhiwa bajaj yake aliyojishindia katika promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa  


  Akizungumza na timu ya ushindi mshindi huyo alielezea furaha yake mara baada kukabidhiwa bajaj na kudai kuwa hiki ndio kipindi cha kuanza mipango mipya yenye kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yake. 
  "Nimefurahi sana kuwa miongoni mwa watu wenye bahati kubwa ya kushinda bajaj, ambayo naamini itanisaidia sana kuboresha maisha yangu vile nimekuwa nikishuhudia wengine wakishinda nilikuwa siamini ila sasa mimi ndio ntakuwa balozi wa SportPesa kwa wale ambao hawaamini kuwa huu ni ukweli" alisema Masoud
  Hata hivyo masoud alisema sababu nyingine iliyomfanya kujiunga na SportPesa ni kutokana na urahisi wa kucheza na mtu anaposhinda haichukui muda kupokea pesa yake ya ubashiri.
  "Kwa sasa nimemaliza upande wa bajaj nguvu yangu naihamishia kwenye jackpot kwani imani yangu ni kuona siku moja nashinda mamilioni ya jackpot hii kwangu itakuwa zaidi ya mabadiliko ntafanya maendeleo makubwa kweli kweli " alisema Masoud
  Akizungumza juu wa ushindi huu Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania Bi. Sabrina Msuya alisema “hata wewe ni mshindi na kumbuka kupanga ni kuchagua na ndio maana wadau walioichagua SportPesa wanashinda kila siku, Ukiweka ubashiri wako na SportPesa kwanza kabisa unaweza kushinda ubashiri wako na kujipatia fedha taslim ama na hata ukikosea ubashiri wako pia unaweza kujiongezea faida kwa kujishindia zawadi mbalimbali”
  Bin Zubeiry
  “Hadi sasa tumekwishatoa jumla ya bajaji 45, ikiwa bajaji 55 zimesalia ningependa kuwahamasisha Watanzania washiriki vilivyo katika promosheni hii yenye lengo la kuinua maisha yao na kiuchumi," amesema Meneja Uhusiano SportPesa Tanzania, Sabrina Msuya. 
  Kama kampuni tunafarijika sana kuona promosheni inaleta manufaa kwa watazania hasa wenye kipato cha chini na kuona wakijitengenezea ajira kupitia bajaji hizi. Kushiriki piga *150*87# j bila kusahau kuweka pesa kwenye akaunti yako na kuweka ubashiri ili upate nafasi ya kushinda.”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PANGANI YATOA TENA MSHINDI PROMOSHENI YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA, SAFARI HII NI MASOUD YUSUPH AJINYAKULIA BAJAJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top