• HABARI MPYA

    Sunday, November 11, 2018

    AKINA MSUVA WAPIGWA 2-1, TENA NYUMBANI NA TIMU ILIYOKUWA INABURUZA MKIA LIGI KUU YA MOROCCO

    Na Mwandishi Wetu, MAZGHAN
    WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Simon Happyod Msuva jana timu yake, Difaa Hassan El-Jadida imechapwa mabao 2-1 nyumbani na FUS Rabat katika mchezo wa Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola Pro Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan. 
    Katika mchezo huo, Msuva alicheza kwa dakika 83 kabla ya kupumzishwa na kumpisha Karim El Hachimi, mabao ya FUS Rabat yakifungwa na Benarif Karim dakika ya 23 na Mekran Abedrrahim dakika ya 39 na Jadida likifungwa na Lahoucine Khoukhouch dakika ya 32.
    Kwa matokeo hayo, FUS Rabat inafikisha pointi sita huo ukiwa ushindi wake wa kwanza katika mechi ya sita, nyingine tatu ikitoa sare na mbili imefungwa na inajinasua mkiani katika Ligi ya timu 16 hadi nafasi ya 13.
    Simon Msuva (kulia) akimpita beki wa FUS Rabat Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan  
    Simon Msuva (kushoto) akitafufa mbinu za kumpita beki wa FUS Rabat Uwanja wa Ben Ahmed El Abdi mjini El Jadida, Mazghan 

    Simon Msuva wa kwanza kulia walioinama katika kikosi cha Difaa Hassan El - Jadida kilichoanza jana   

    Difaa Hassan El- Jadidi yenyewe inabaki nafasi ya nne na pointi zake 10, ikicheza mechi ya tano  ya msimu na inazidiwa pointi tat utu na vinara, Hassania Agadir waliocheza mechi mbili zaidi. 
    Kikosi cha Difaa Hassan El – Jadidi kilikuwa; Mohamed El Yousfi, Tarik Astati, Saad Lagrou, Marouane Hadhoudhi, Youssef Agourdeoum, Mohammed Ali Bemammer, El Mehdi Karnass, Simon Msuva/Karim El Hachimi dk83, Ayoub Nanah/Bilal El Magri dk64, Lahoucine Khoukhouch na Adnane El Quadry.
    FUS Rabat; Amsif Mohammed, Said Mohamed, Bach Anas,  El Bassil Mehdi, Louani Amine, Skouma Ayoub, Makrane Abedrrahim, Zerhouni Nawfel, Benarif Karim, El Bahraoui Ibrahim na Ait Khoursa Saad.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AKINA MSUVA WAPIGWA 2-1, TENA NYUMBANI NA TIMU ILIYOKUWA INABURUZA MKIA LIGI KUU YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top