• HABARI MPYA

  Tuesday, November 06, 2018

  AL AHLY KUMKOSA AZARO MARUDIANO NA ESPERANCE IJUMAA

  MSHAMBULIAJI Mmorocco wa Al Ahly ya Misri, Walid Azaro ataukosa mchezo wa marudiano wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Ijumaa dhidi ya wenyeji, Esperance Uwanja wa Olimpiki mjini Rades.
  Hiyo ni baada ya kufungiwa mechi mbili na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) katika kikao chake cha Novemba 5, mwaka huu.
  Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Nidhamu ya CAF, Raymond Hack amesema Azaro atakosa mechi mbili zijazo za Al Ahly, ya kwanza ni hiyo dhidi ya Esperance baada ya makosa aliyoyafanya kwenye mchezo wa kwanza.  Walid Azaro atakosa mchezo wa marudiano fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Esperance Ijumaa 

  Pamoja na kufungiwa mechi mbili, klabu yake Al Ahly ambayo ilishinda 3-1 kwenye mechi ya kwanza Ijumaa iliyopita Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria, nayo imepigwa faini ya dola za Kimarekani 20, 000. 
  Kwa ushindi huo uliotokana na mabao mawili ya Walid Soliman dakika za 34 na 76 na lingine Amr El Sulya dakika ya 58, Ahly watahitaji sare au kufungwa kwa tofauti ya bao moja tu katika mchezo wa marudiano Novemba 9 mjini Tunis ili kutwaa taji la tisa la rekodi la Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Esperance ambayo siku hiyo bao lake lilifungwa na Youcef Belaili dakika ya 64, itahitaji ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Ijumaa mjini Rades ili kutwaa taji hilo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AL AHLY KUMKOSA AZARO MARUDIANO NA ESPERANCE IJUMAA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top