• HABARI MPYA

  Sunday, November 05, 2017

  YANGA WALIA NA HALI HEWA SINGIDA ILIWAKOSESHA USHINDI

  Na Salma Suleiman, SINGIDA
  KOCHA Msaidizi wa Yanga SC, Nsajigwa Shadrack Joel Mwandemele amesema kwamba hali ya hewa ya Singida iliwakosesha ushindi jana.
  Yanga ililazimishwa sare ya bila mabao na wenyeji, Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Namfua mjini Singida jana.
  Na baada ya mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Yanga, Nsajigwa ambaye ni beki na Nahodha wa zamani wa klabu hiyo alisema upepo mkali wa Singida jana uliwakosesha ushindi. 
  Kocha Msaidizi wa Yanga SC, Nsajigwa Shadrack (kushoto) akiwa na bosi wake, Mzambia George Lwandamina (kulia) 

  “Tulihitaji ushindi, lakini matarajio yetu yameenda tofauti, kipindi cha kwanza Singida walitusumbua sana, lakini baadaye tuliweza kwenda nao sawa. Vilevile hali ya hewa ya upepo ilichangia kwa kiasi fulani, kwani mipira ilikuwa inakwenda tofauti na ulivyokuwa inapigwa,”alisema.
  Sare hiyo ya pili mfululizo baada ya Jumamosi iliyopita pia kutoka 1-1 na mahasimu wao wa jadi, Simba inaifanya Yanga ifikishe pointi 17 baada ya kucheza mechi tisa, wakati Singida inafikisha pointi 14 baada ya mechi tisa pia.
  Na baada ya Azam FC kushinda 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana, inapanda kileleni kutokana na kufikisha pointi 19, ingawa leo inaweza kuteremka nayo iwapo Simba itashinda. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WALIA NA HALI HEWA SINGIDA ILIWAKOSESHA USHINDI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top