• HABARI MPYA

  Sunday, November 05, 2017

  PLUIJM AUSIFU UWANJA WA NAMFUA ASEMA NI ZAIDI YA JAMHURI

  Na Salma Suleiman, SINGIDA
  KOCHA Mkuu wa Singida United, Mholanzi Hans van der Pluijm amesema timu yake sasa inacheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara katika Uwanja mzuri wa Namfua na hiyo itakuwa chachu ya kupata matokeo mazuri. 
  Pluijm aliyasema hayo baada ya sare ya 0-0 dhidi ya timu yake ya zamani, Yanga SC katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu kufanyika Uwanja wa Namfua mkoani Singida msimu huu.
  Mholanzi huyo alisema Uwanja wa Namfua ni mzuri kuliko wa Jamhuri mkoani Dodoma ambao walikuwa wanautumia kwa mechi zao zilizotangulia za nyumbani za Ligi Kuu.
  Hans van der Pluijm (kushoto) akizungumza na mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa jana Singida
  “Uwanja wa Namfua umekuwa mzuri zaidi baada ya marekebisho ukilinganisha na wa Jamhuri Dodoma tuliokuwa tunautumia mwanzo,”alisema.
  Akizungumzia kushindwa kupata ushindi jana wakicheza nyumbani kwa mara ya kwanza tangu wapande Ligi Kuu msimu huu, Pluijm alisema kwamba mechi ilikuwa ngumu na kila timu ilipambana kuhakikisha inashinda.
  “Kucheza na timu kubwa kama Yanga kunakuwa na changamoto nyingi. Nia yetu ilikuwa kubuka na ushindi katika mchezo huo, lakini bahati haikuwa yetu, wachezaji wetu walicheza vizuri, lakini safu ya kiungo ya Yanga ilikuwa makini na kutibua mipango yetu,”alisema.

  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AUSIFU UWANJA WA NAMFUA ASEMA NI ZAIDI YA JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top