• HABARI MPYA

  Monday, November 06, 2017

  WEST HAM YAMFUKUZA BILIC, MOYES KUCHUKUA NAFASI

  West Ham imemfukuza kocha Slaven Bilic baada ya matokeo mabaya PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  REKODI YA SLAVEN BILIC WEST HAM UTD

  Mechi: 111 | Kushinda: 42 | Sare: 30 | Kufungwa: 39
  Asilimia ya ushindi: 37.84 
  KOCHA Slaven Bilic amefukuzwa West Ham United baada ya matokeo mabaya.
  The Hammers imeshinda mechi mbili tu kati ya zote za Ligi Kuu ya England msimu wote na wanakwenda kwenye mapumziko ya mechi za kimataifa wakiwa kwenye nafasi za mkiani, baada ya kufungwa 4-1 na Liverpool Jumamosi.
  Bin Zubeiry Sports - Online inafahamu kwamba The Hammers wanataka kumteua David Moyes kuchukua nafasi ya Bilic hadi mwishoni mwa msimu.
  Wengine wanaowania kiti hicho ni kocha wa zamani wa Manchester City, Roberto Mancini na Alan Pardew - ambaye atakuwa anarudi kama akipewa nafasi hiyo, baada ya awali kufanya kazi The Hammers kati ya mwaka 2003 na 2006.
  Taarifa ya West Ham imesema: "West Ham United inaweza kuthibitisha kwamba Slaven Bilic leo ameondoka kwenye nafasi yake katika klabu,".
  "Mwenyekiti na bodi ya West Ham United wangependa kutoa shukrani za dhati kwa Slaven na timu yake kwa huduma zao kwa miaka miwili na nusu iliyopita, lakini amini mabadiliko ni kawaida sasa ili klabu isonge mbele na kutimiza malengo yake,".
  Bilic alianza kazi West Ham mwaka 2015 na akaiwezesha kushika nafasi ya saba katika msimu wake wa kwanza.
  Lakini Mcroatia huyo akashindwa kurudia mafanikio ya msimu uliotangulia na West Ham ikaangukia katikati ya msimamo wa Ligi.
  Amefukuzwa pamoja na benchi lake lote la ufundi Uwanja wa London, akiwemo mchezaji wa zamani maarufu, Julian Dicks. West Ham itasafiri kwenda Uwanja wa Vicarage Road kumenyana na Watford baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa. 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WEST HAM YAMFUKUZA BILIC, MOYES KUCHUKUA NAFASI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top