• HABARI MPYA

  Thursday, November 09, 2017

  TIMU DARAJA LA PILI ZASHINDILIWA ADHABU KWA MAOSA TOFAUTI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Pepsi imepigwa faini ya sh. 100,000 kwa kuchelewa kwenye kikao cha maandalizi ya mechi namba 1 ya Kundi B Ligi Daraja la Pili dhidi ya Madini, timu hizo zikitoka sare ya kufungana bao 1-1 na pia kuchelewa kufika uwanjani. 
  Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya Habari Jumatano imesema kwamba, adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
  Mechi namba 9 Kundi B (Madini 1 v Kilimanjaro Heroes 1). Kilimanjaro Heroes imepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kikao cha maandalizi (pre match meeting) kwa dakika 16. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
  Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidao

  Mechi namba 11 Kundi B (Kilimanjaro Heroes 1 v African Sports 1). African Sports imepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kufika uwanjani, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(9) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Taratibu za Mchezo. Kanuni hiyo inatika timu kufika uwanjani dakika 60 kabla ya mechi kuanza. Mechi namba 4 Kundi C (Green Warriors 1 v Mkamba Rangers 0). Klabu ya Mkamba Rangers imepewa Onyo Kali kutokana na timu yake kutohudhuria kikao cha maandalizi ya mechi, kitendo ambacho ni kinyume na Kanuni ya 14(2b) ya Ligi Daraja la Kwanza. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
  Mechi namba 5 Kundi D (Milambo 1 v Area C 0). Milambo imepewa Onyo Kali kwa kuwakilishwa na maofisa pungufu kwenye kikao cha maandalizi ya mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
  Mechi namba 12 Kundi D (Milambo 0 v Mashujaa 1). Milambo imepewa Onyo Kali kwa kuwakilishwa na maofisa pungufu kwenye kikao cha maandalizi ya mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili.
  Pia Mwamuzi wa Akiba, Rajab Said amepewa Onyo Kali kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha maandalizi ya mechi kwa dakika 6. Adhabu ya Mwamuzi ni kwa mujibu wa Kanuni ya 83(5) ya Ligi Daraja la Pili kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
  Mechi namba 15 Kundi D (Area C 1 v Mashujaa 0). Mashujaa imepewa Onyo Kali kwa kutohudhuria   kikao cha maandalizi ya mechi. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(3) ya Ligi Daraja la Pili. Vilevile timu ya Mashujaa imepigwa faini ya sh 200,000 (laki mbili) kwa kupitia mlango usio rasmi wakati wa kuingia uwanjani. Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(140 ya Ligi Daraja la Pili.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU DARAJA LA PILI ZASHINDILIWA ADHABU KWA MAOSA TOFAUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top