• HABARI MPYA

  Friday, November 03, 2017

  SIMBA WAFUATA POINTI SITA MBEYA KWA NDEGE, MSIMU HUU UBINGWA KAZI IPO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Simba kinaondoka asubuhi hii kwa ndege kwenda Mbeya kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania dhidi ya wenyeji Mbeya City, Jumapili Uwanja wa Sokoine.
  Wachezaji wote wanasafiri isipokuwa majeruhi watatu, kipa Said Mohammed ‘Nduda’, mabeki Shomary Kapombe na Salim Mbonde ambao ni majeruhi kwa sasa.
  Simba SC itakaa karibu nusu mwezi Mbeya kwa sababu mbali ya mchezo wa keshokutwa, itakuwa na mchezo mwingine wa Ligi Kuu Novemba 18 dhidi ya Tanzania Prisons.   
  Na uongozi umepanga kuwa na mchezo wa kirafiki wiki ijayo baada ya mchezo wake wa kwanza dhidi ya Mbeya City Jumapili.
  Kwa ujumla, Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea leo, Maji Maji FC wakiikaribisha Stand United Uwanja wa Maji Maji mjini Songea, wakati kesho mabingwa watetezi, Yanga watakuwa wageni wa Singida United Uwanja wa Namfua, Singida na Ndanda FC wataikaribisha Mtibwa Sugar Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
  Mechi nyingine za Jumamosi, Kagera Sugar wataikaribisha Tanzania Prisons Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Njombe Mji FC wataikaribisha Mbao FC Uwanja wa Saba Saba na Azam FC watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Na Jumapili mbali na Mbeya City kuwa wenyeji wa Simba, Lipuli FC nao wataikaribisha Mwadui FC Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA WAFUATA POINTI SITA MBEYA KWA NDEGE, MSIMU HUU UBINGWA KAZI IPO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top