• HABARI MPYA

    Wednesday, November 01, 2017

    SAMATTA ATEULIWA KUWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ni miongoni mwa wachezaji 30 walioteuliwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika.
    Shirikisho la Soka Afrika (CAF) pia limetaja orodha ya wachezaji 30 wengine kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Anayecheza Afrika.
    Washindi wa tuzo zote watatokana na kura za Makocha Wakuu nanWakurugenzi wa Ufundi wa vyama na mashirikisho ya Soka wanachama wa CAF pamoja na jopo la wataalamu kutoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali Afrika.
    Mbwana Samatta ameteuliwa kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka Afrika 2017

    Sherehe za tuzo zinatarajiwa kufanyika Alhamisi ya Januari 4 mwaka 2018 mjini Accra, Ghana.
    Samatta anayechezea KRC Genk ya Ugelbiji, amewahi kuwa Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka juzi, wakati huo anachezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye aliiwezesha kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika.
    Wachezaji wengine wa Afrika Mashariki walioingia katika kinyang’anyiro cha tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika mwaka huu ni mshambuliaji Mkenya, Michael Olunga wa Girona ya Hispania na kipa Mganda, Denis Onyango wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini. 

    WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFFRIKA

    African Player of the Year
    1. Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)
    2. Bertrand Traore (Burkina Faso & Lyon)
    3. Cedric Bakambu (DRC & Villareal)
    4. Christian Atsu (Ghana & Newcastle)
    5. Christian Bassogog (Cameroon & Henan Jianye)
    6. Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
    7. Eric Bailly (Ivory Coast & Manchester United)
    8. Essam El Hadary (Misri & Al Taawoun)
    9. Fabrice Ondoa (Cameroon & Sevilla)
    10. Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco)
    11. Jean Michel Seri (Ivory Coast & Nice)
    12. Junior Kabananga (DRC & Astana)
    13. Karim El Ahmadi (Morocco & Feyenoord)
    14. Keita Balde (Senegal & Monaco)
    15. Khalid Boutaib (Morocco & Yeni Malatyaspor)
    16. Mbwana Samata (Tanzania & Genk)
    17. Michael Olunga (Kenya & Girona)
    18. Mohamed Salah (Misri & Liverpool)
    19. Moussa Marega (Mali & Porto)
    20. Naby Keita (Guinea & RB Leipzig)
    21. Percy Tau (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns)
    22. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)
    23. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)
    24. Thomas Partey (Ghana & Atletico Madrid)
    25. Victor Moses (Nigeria & Chelsea)
    26. Vincent Aboubakar (Cameroon & Porto)
    27. William Troost-Ekong (Nigeria & Bursaspor)
    28. Yacine Brahimi (Algeria & Porto)
    29. Youssef Msakni (Tunisia & Al Duhail)
    30. Yves Bissouma (Mali & Lille)


    TUZO YA MWANASOKA BORA ANAYECHEZA AFRIKA
    1. Achraf Bencharki (Morocco & Wydad Athletic Club)
    2. Ahmed Fathi (Misri & Al Ahly)
    3. Alkhaly Bangoura (Guinea & Etoile du Sahel)
    4. Ali Maaloul (Tunisia & Al Ahly)
    5. Aristide Bance (Burkina Faso & Al Masry)
    6. Ayman Majid (Morocco & FUS Rabat)
    7. Aymen Mathlouthi (Tunisia & Etoile du Sahel)
    8. Ben Malango (DRC & TP Mazembe)
    9. Dean Furman (Africa Kusini & Supersport United)
    10. Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)
    11. Elsamani Saadeldin (Sudan & Al Merreikh)
    12. Fackson Kapumbu (Zambia & Zesco)
    13. Fawzi Chaouchi (Algeria & MC Alger)
    14. Geoffrey Serunkuma (Uganda & KCCA)
    15. Jeremy Brockie (New Zealand & Supersport)
    16. Junior Ajayi (Nigeria & Al Ahly)
    17. Karim Aouadhi (Tunisia & CS Sfaxien)
    18. Mohamed Meftah (Algeria & USM Alger)
    19. Mohamed Ounnajem (Morocco & Wydad Athletic Club)
    20. Muaid Ellafi (Libya & Ahly Tripoli)
    21. Nasr Eldin Ahmed (Sudan & Hilal Obeid)
    22. Oussama Darfalou (Algeria & USM Alger)
    23. Percy Tau (Afrika Kusini & Mamelodi Sundowns)
    24. Sabelo Ndzinisa (Swaziland & Mbabane Swallows)
    25. Saber Khalifa (Tunisia & Club Africain)
    26. Saladin Said (Ethiopia & Saint George)
    27. Sylvain Gbohouo (Ivory Coast & TP Mazembe)
    28. Tady Etekiama (DRC & AS Vita)
    29. Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance)
    30. Tarek Hamed (Misri & Zamalek)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA ATEULIWA KUWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top