• HABARI MPYA

    Sunday, November 05, 2017

    NINJA WA YANGA AITWA KIKOSI CHA ZANZIBAR KOMBE LA CHALLENGE

    Na Salum Vuai, ZANZIBAR
    BEKI mpya wa Yanga SC, Abdallah Hajji 'Ninja' ni miongoni mwa wachezaji 30 walioitwa kwenye kikosi cha awali cha timu ya taifa ya Zanzibar, maarufu Zanzibar Heroes kwa ajili ya michuano ya CECAFA Challenge mwezi ujao.  
    Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limetangaza kurudi kwa Kombe la Challenge na Kocha Mkuu wa Zanzibar Heroes, Hemed Suleiman 'Morocco', leo ametaja kikosi cha awali, akichukua nyota kadhaa wanaocheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Kwa mujibu wa CECAFA, mashindano hayo yatafanyika kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya.
    Wachezaji hao watafanya mazoezi ya pamoja na baadae kuchujwa ili kupata kikosi cha mwisho kitakachokwenda kujaribu kutwaa ubingwa wa pili kwa Zanzibar katika historia ya mashindano hayo.
    Abdallah Hajji 'Ninja' ni miongoni mwa wachezaji 30 walioitwa kwenye kikosi cha awali cha Zanzibar Heroes kwa ajili ya Challenge

    Mara ya kwanza na pekee Zanzibar kutwaa taji la patashika hizo, ilikuwa mwaka 1995 wakati michuano hiyo ilipofanyika nchini Uganda.
    Zanzibar Heroes ambayo wakati huo ilikuwa ikinolewa na kocha Hafidh Badru akisaidiwa na Shaaban Ramadhani, ilitawazwa ubingwa baada ya kuichapa Uganda bao 1-0 lililowekwa kimiani na Victor Bambo.
    Wanandinga hao wateule ni makipa; Ahmed Ali ‘Salula’ (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi) na Mohammed Abdulrahman ‘Wawesha’ (JKU).
    Mabeki ni; Abdallah Haji ‘Ninja’ (Yanga), Mohammed Othman Mmanga (Polisi), Ibrahim Mohammed ‘Sangula’ (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh ‘Machupa’ (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame ‘Luiz’ (Mlandege), Issa Haidar ‘Mwalala’ (JKU), Abdulla Kheir ‘Sebo’ (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).
    Viungo Abdul-Samad Kassim (Miembeni City), Abdulaziz Makame (Taifa ya Jang’ombe), Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma ‘Zimbwe’ (Chipukizi), Mohammed Issa ‘Banka’ (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman ‘Pwina’ (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Ali Yahya (Akademi ya Hispania), Hamad Mshamata (Chuoni) na Suleiman Kassim ‘Selembe’ (Majimaji).
    Washambuliaji ni; Kassim Suleiman (Prisons), Matteo Anthony (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa ‘Rais’ (Jang’ombe Boys),
    Mwalimu Mohammed (Jamhuri) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).
    Katika hatua nyengine, Moroko ametaja kikosi cha timu ya soka la wanawake Zanzibar Queens, ambacho pia kitashiriki michuano ya Chalenji itakayofanyika nchini Rwanda kikiwa na wachezaji 20.
    Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika wakati wowote ndani ya mwezi huu wa Novemba.
    Hata hivyo, Moroko sie mwalimu wa timu hiyo bali amesaidia kufanya uteuzi wa wanadada hao huku kocha wake akitarajiwa kutajwa hapo baadae.
    Makipa ni; Salma Abdallah (Green Queens), Hajra Abdallah (Jumbi) na Mtumwa (New Generation Queens).
    Walinzi ni; Hawa Ali (New Generation Queens), Mtumwa Khatib (Women Fighters), Aziza Mwadini (New Generation Queens), Flora Kayanda (Jumbi), Safaa Makirikiri (New Generation Queens) na
    Neema Suleiman (Jumbi).
    Viungo ni; Mwajuma Ali (Jumbi), Nasrin Mohammed (Women Fighters), Riziki Abdallah ‘Chadole’ (Jumbi), Aziza Ali (Jumbi) na Sijali Abdallah (Green Queens).
    Washambuliaji ni; Mwajuma Abdallah (New Generation Queens), Shadida Abdallah (Women Fighters), Neema Machano (Jumbi), Dawa Haji (Women Fighters), Sabah Hashim ‘Messi’ (New Generation Queens) na Grace Ronald (Green Queens).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NINJA WA YANGA AITWA KIKOSI CHA ZANZIBAR KOMBE LA CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top