• HABARI MPYA

  Sunday, November 05, 2017

  MAN CITY 'YAIKOKOMEKA' ARSENAL 3-1 ETIHAD, MOJA LA OFFSIDE

  Mfungaji bora mpya wa kihistoria wa Manchester City, Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia timu yake bao la pili kwa penalti dakika ya 50 baada ya Nacho Monreal kumchezea rafu Raheem Sterling katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Arsenal leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Etihad. Mabao mengine ya Man City yamefungwa na Kevin de Bruyne dakika ya 19 na Gabriel Jesus dakika ya 74, ingawa alikuwa ameotea wakati la Arsenal limefungwa na Alexandre Lacazette dakika ya 65 baada ya kutokea benchi kuchukua nafasi ya Francis Coquelin dakika ya 56 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN CITY 'YAIKOKOMEKA' ARSENAL 3-1 ETIHAD, MOJA LA OFFSIDE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top