• HABARI MPYA

  Thursday, November 09, 2017

  KESSY: DHAMIRA YA YANGA NI KUTETEA UBINGWA

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kulia wa Yanga, Hassan Ramadhani ‘Kessy’ amesema kwamba pamoja na changamoto zinazowakabili kwa sasa, lakini dhamira inabaki pale pale, kutetea ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online jana, Kessy amesema kwamba Ligi Kuu bado ipo katika hatua za awali mno, hivyo ni mapema kuanza kubashiri bingwa.
  Kessy amesema hadi sasa mwenendo wa Yanga si mbaya kwenye Ligi Kuu, isipokuwa tu msimu huu unaonekana utakuwa na ushindani zaidi.
  Amesema timu zilizoibuka na ushindi katika raundi ya tisa zinaweza kukwama katika raundi ijayo, wakati zilizokwama raundi iliyopita zinaweza kuibuka raundi ya 10.
  “Ndiyo hivyo, yaani kuna timu unacheza nayo hata wewe mwenyewe ukipata sare unashukuru, lakini kuna timu nyingine ukitoka nayo sare unajilaumu. Singida ni kati ya timu ngumu msimu huu zimesajili vizuri na zina motisha nzuri kwa wachezaji wake na hamasa kubwa,”amesema.
  Yanga inaendelea na mazoezi mjini  Dar es Salaam kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu, baada ya Jumamosi ya wiki iliyopita kulazimishwa sare ya 0-0 na wenyeji, Singiza United Uwanja wa Namfua, Singida.
  Mabingwa hao mara tatu mfululizo, wanatarajiwa kuteremka tena dimbani, Novemba 19 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kumenyana na Mbeya City.    
  Kwa sasa Yanga inashika nafasi ya tatu katika Ligi Kuu kwa pointi zake 17, baada ya kucheza mechi tisa, ikiwa nyuma ya Simba na Azam FC zenye pointi 19 kila mmoja baada ya kucheza mechi tisa pia.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KESSY: DHAMIRA YA YANGA NI KUTETEA UBINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top