• HABARI MPYA

  Thursday, November 02, 2017

  AGUERO AVUNJA REKODI YA MABAO MAN CITY IKIIPIGA NAPOLI 4-2 ITALIA

  Mshambuliaji Sergio Aguero akishangilia baada ya kuifungia Manchester City bao la tatu dakika ya 69 katika ushindi wa 4-2 dhidi ya wenyeji, Napoli usiku wa Jumatano Uwanja wa San Paolo mjini Napoli, Italia katika mchezo wa Kundi F Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuvunja rekodi ya kufunga mabao mengi kihistoria katika timu hiyo iliyowekwa na Eric Brook aliyefunga mabao 177 miaka ya 1930. Mabao mengine ya City yamefungwa na Nicolas Otamendi dakika ya 34, John Stones dakika ya 48 na Raheem Sterling dakika ya 90 na ushei, wakati ya Napoli yamefungwa na Lorenzo Insigne dakika ya 21 na Jorginho kwa penalti dakika ya 62 kufuatia Leroy Sane kumchezea rafy Raul Albiol kwenye boksi PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AGUERO AVUNJA REKODI YA MABAO MAN CITY IKIIPIGA NAPOLI 4-2 ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top