• HABARI MPYA

  Thursday, March 16, 2017

  ZANZIBAR SASA MWANACHAMA KAMILI CAF

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA) kimepata uanachama kamili wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa mujibu wa habari kutoka Addis Ababa, Ethiopia.
  Kwa maana hiyo, Zanzibar inatengana moja kwa moja moja Tanzania Bara katika mashindano yote ya CAF.
  Mkutano Mkuu wa 39 wa CAF unaoendelea mjini Addis Ababa, Ethiopia tangu jana umeafiki kuipa Zanzibar uanachama kamili baada ya awali kuipa uanachama wa muda kama mwanachama mshiriki.
  ZFA ilianzishwa mwaka mwaka 1949 na kipindi chote mbali ya kuwa sehemu ya Tanzania kisoka, imekuwa ikishiriki michuano ya Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) tu kama nchi. 
  Katika hatua nyingine, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limempongeza Rais mpya wa CAF, Ahmad Ahmad baada ya kumshinda rais wa muda mrefu, Issa Hayatou kwa kura 34 kwa 20.
  Loading...
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZANZIBAR SASA MWANACHAMA KAMILI CAF Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top