• HABARI MPYA

  Thursday, March 16, 2017

  WATANZANIA WAOMBWA KUICHANGIA SERENGETI BOYS KUPITIA NAMBA HII MITANDAO YOTE

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  WATANZANIA wameombwa kuichangia timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys kupitia namba 223344 kwa ajili ya maandalizi yake ya kushiriki Fainali za Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon.
  Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano wa Airtel, Beatrice Singano ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Kusaidia Serengeti Boys katika Mkutano na Waandishi wa Habari Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
  “Kwa kila mwenye moyo wa kuchangia anaweza kuchangia kupitia namba 223344 na namba hii itatumika katika mitandao mitatu ambayo ni Airtel, Tigo pamoja na Vodacom.  Na jinsi ya kulipia utalipia kwa njia ya Selcom malipo kupitia mtandao husika, kupitia mtandao wa Airtel unapiga *150*60# na tigo *150*01# na Vodacom *150*01#”alisema Beatrice.
  Beatrice Singano akizungumza na Waandishi wa Habari Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo

  Mwenyekiti wa Kamati ya Serengeti Boys, Charles Hillary akizungumza leo

  Amesema pia kutokana na umahiri Serengeti Boys waliouonyesha katika michezo ya awali ana uhakika timu hiyo itafanya vizuri katika fainali hizo, hivyo kuwataka Watanzania kuwa bega kwa bega na kikosi hicho.
  Mapema kwenye mkutano huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Charles Hillary alisema kwamba wameorodhesha makampuni mbalimbali waliyoyaomba kuichangia Serengeti Boys.
  Hillary amesema kwamba watabisha hodi pia na Halmashauri za Wilaya zote nchini kwa msaada wa Serikali na huko wanatarajia kupata Sh.Milioni 100.
  Na akasema si wote watakiwa kuchangia fedha, bali wengine watatoa misaada mingine inayohitajika wakati wa maandalizi ya timu kwenda Fainali za Gabon, ikiwemo tiketi za ndege, kambi, vyakula na kadhalika. 
  Serengeti Boys ipo kambini kwa wiki mbili sasa katika hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kikiendelea na maandalizi ya michezo miwili ya kirafiki itakayo chezwa mkoani Kagera kabla ya kwenda mjini Rabat, Morocco kwa kambi ya mwezi mmoja ikiwa ni maandalizi ya fainali za vijana wenye umri chini ya miaka 17 zitakazo fanyika nchini Gabon Mei 14 mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WATANZANIA WAOMBWA KUICHANGIA SERENGETI BOYS KUPITIA NAMBA HII MITANDAO YOTE Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top