• HABARI MPYA

    Thursday, March 16, 2017

    AHMAD AHMAD NDIYE RAIS MPYA WA CAF, HAYATOU NJE

    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) leo limeandika historia mpya kufuatia kupata rais mpya, Ahmad Ahmad wa Madagascar aliyemuangusha Issa Hayatou aliyedumu kwa miaka 29 ofisini.
    Ahmad, Mkuu wa Shirikisho la Soka la Madagascar, ameshinda Urais wa CAF katika uchaguzi uliofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopian kwa kuzoa kura 34 huku Hayatou akiambulia 20.
    Ahmad Ahmad wa Madagascar amemuangusha Issa Hayatou aliyedumu kwa miaka 29 CAF

    Ahmad, mwenye umri wa miaka 57, baba wa watoto wa wawili alikuwa mchezaji kabla ya kuwa kocha na baadaye kiongozi wa soka wa Madagascar tangu mwaka 2003.
    Wazi Ahmad amebebwa na kiu kubwa ya mabadiliko ya viongozi wa vyama vya Afrika ndani ya CAF na kwa ujumla wadau wengi wa mchezo huo barani walimchoka Hayatou, raia wa Cameroon aliyeongoza CAF tangu mwaka 1988 na Makamu wa Rais wa FIFA. 
    Hayatou (kulia) akiwa na Rais wa zamani wa FIFA, Sepp Blatter (kushoto) 

    Hayatou atakumbukwa kwa jitihada zake za kukuza soka ya Afrika, ikiwemo kuongeza nafasi ya timu za bara hili kwenye fainali za Kombe la Dunia kutoka tatu hadi tano na pia kuongeza fedha kwenye michuanoa ya barani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AHMAD AHMAD NDIYE RAIS MPYA WA CAF, HAYATOU NJE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top