• HABARI MPYA

    Saturday, March 18, 2017

    BONNY, GARDEL WATEMWA KIKOSI CHA TEMBO WA IVORY COAST

    WASHAMBULIAJI waliopoteza makali katika Ligi Kuu ya England, Wilfried Bony na Max Gradel wametemwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ivory Coast kilichotajwa jana na kocha wa muda, Ibrahim Kamara kufuatia matokeo mabaya kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
    Bony, aliyeichezea mechi 51 Ivory Coast, anayecheza kwa mkopo Manchester City, na Gradel wa Bournemouth, ambaye ameichezea mechi 45 timu hiyo, wameenguliwa kwenye kwenye kikosi cha wachezaji 23 walioitwa kwa ajili ya mechi za kirafiki dhidi ya Urusi na Senegal na baadaye mwezi huu.
    Wachezaji sita waliokuwapo kwenye kikosi cha timu hiyo kilichotolewa Raundi ya Kwanza Fainali za Mataifa ya Afrika wametemwa akiwemo Salomon Kalou wa Hertha Berlin, ambaye tayari ametangaza kustaafu soka ya kimataifa.
    Kamara, aliyechukua nafasi ya Michel Dussuyer baada ya AFCON, amewarejesha Roger Assale, Cyriac Gohi Bi na Abdoul Karim Cisse wakati pia amewaita kwa mara ya kwanza Cheick Ibrahim Comara wa AFAD Abidjan na Moussa Kone, ambao wanacheza Cesena ya Italia.
    Ivory Coast itamenyana na Urusi mjini Krasnodar Machi 24 na Senegal mjini Paris siku tatu baadaye.
    Kikosi kamili cha Tembo hao wa Ivory Coast ni; Sylvain Gbohouo (TP Mazembe/DRC), Ali Badra Sangaré (AS Tanda/Ivory Coast), Abdoul Karim Cissé (SC Gagnoa/Ivory Coast)
    Mabeki: Serge Aurier (Paris SG/Ufaransa), Mamadou Bagayoko (St Truiden/Ubelgiji), Eric Bailly (Man Utd/England), Abdoulaye Bamba (Angers/Ufaransa), Simon Deli (Slavia Prague/Jamhuri ya Czech), Wilfried Kanon (Den Haag/Uholanzi), Adama Traore (Basel/Uswisi), Cheick Ibrahim Comara (AFAD/Ivory Coast)
    Midfielders: Cheick Doukoure (Metz/Ufaransa), Jules Christ Kouassi Eboué (Celtic/Scotland), Franck Kessié (Atalanta/Italia), Geoffroy Serey Die (Basel/Uswisi), Jean Michael Seri (Nice/Ufaransa), Moussa Kone (Cesena/Italia)
    Washambuliaji: Nicolas Pepe (Angers/Ufaransa), Jonathan Kodjia (Aston Villa/England), Giovanni Sio (Rennes/Ufaransa), Roger Assale (Young Boys/Uswisi), GOHI BI Cyriac Gohi Bi (Fulham/England), Wilfried Zaha (Crystal Palace/England).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BONNY, GARDEL WATEMWA KIKOSI CHA TEMBO WA IVORY COAST Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top