• HABARI MPYA

  Saturday, March 18, 2017

  NIYONZIMA, CHIRWA NA MSUVA WAANZISHWA YANGA KUISHAMBULIA ZANACO LEO

  Na Jeff Leah, LUSAKA
  KIUNGO Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima anaanza leo katika mchezo wa marudiano wa hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Zanaco Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka.
  Pamoja na Niyonzima ambaye hajacheza tangu Februari 25, Yanga ilipofungwa 2-1 na mahasimu, Simba, kocha George Lwandamina pia amewapanga Mzambia mwenzake, Justin Zulu na Mzimbabwe Thabani Kamusoko kucheza pamoja na Niyonzima katika safu ya kiungo.
  Mawinga Simon Msuva na Mzambia Obrey Chirwa leo watacheza kama washambuliaji wakati na pembeni kushoto atakuwapo Mwashiuya na kulia Niyonzima. 
  Haruna Niyonzima anaanza leo katika mechi na Zanaco Uwanja wa Taifa wa Mashujaa, Lusaka

  Ikumbukwe Yanga imekwenda Zamba abila mshambuliaji hata mmoja, baada ya washambuliaji wake wote wanne, Mrundi Amissi Tambwe, Mzimbabwe Donald Ngoma na wazalendo Malimi Busungu na Matheo Anthony kubaki Dar es Salaam kwa sababu ni majetuhi,
  Kwa ujumla kikosi cha Yanga leo kipo hivi; Deo Munishi ‘Dida’, Hassan Kessy, Mwinyi Hajji, Kevin Yondani, Vincent Bossou, Justin Zulu, Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Simon Msuva, Obrey Chirwa na Geoffrey Mwashiuya.
  Katika benchi watakuwapo Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Andrew Vincent ‘Dante’, Said Juma 'Makapu', Juma Mahadhi, Emannuel Martin na Deus Kaseke.
  Yanga inahitaji ushindi lazima jioni ya leo ili kuingia hatua ya makundi, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam. Ikumbukwe timu itakayotolewa, itaingia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIYONZIMA, CHIRWA NA MSUVA WAANZISHWA YANGA KUISHAMBULIA ZANACO LEO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top