• HABARI MPYA

    Friday, March 03, 2017

    SIMBA NA MBEYA CITY KESHO HAPATOSHI TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi vinara wa ligi hiyo Simba inatarajiwa kuialika Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ukiacha mchezo huo, michezo mingine ya kesho Jumamosi Machi 4, mwaka huu itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
    Azam FC pia itacheza Jumamosi Machi 4, mwaka huu na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi. Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni wakati mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.
    Jumapili Machi 5, mwaka huu Mtibwa Sugar itaialika Young Africans kwenye uwanja huo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utachezwa Uwanja wa Uhuru ambako African Lyon itaialika Mwadui ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona siku ya Jumatatu Machi 6, mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA MBEYA CITY KESHO HAPATOSHI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top