• HABARI MPYA

  Friday, March 03, 2017

  SERENGETI BOYS KUTEMBELEA WANAOPAMBANA KUACHA 'UTEJA' KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ya Vijana wa Tanzania wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’, kesho Jumamosi tarehe 04 Machi, 2017, watatembelea Kituo cha vijana wanaopatiwa matibabu baada ya kuathirika na dawa za kulevya.
  Kituo hicho kinachoitwa Sober House kipo Bagamoyo mkoani Pwani. Ni kituo maalumu kwa tiba ya vijana kinaendeshwa na kusimamiwa na Shirika la Life and Hope Rehabilitation Centre chini ya Mkurugenzi, Al-Karim Bhanji.
  Ikiwa huko, vijana wa Serengeti Boys ambao kwa sasa wako kwenye kipindi cha mabadiliko ya katika sayansi ya mwili hivyo itakuwa somo kubwa kwao katika kujielimisha kuhusu mustakabali wa maisha yao.
  Kwa upande wa TFF kuwapeleka vijana hao huko ni utekelezaji Kanuni ya 36 (7) ya Ligi Kuu ya Vodacom inayozungumza kukataa rushwa, madawa, ubaguzi, fujo, kamari na mambo mengine ya hatari kwa mchezo wa mpira wa miguu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS KUTEMBELEA WANAOPAMBANA KUACHA 'UTEJA' KESHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top