• HABARI MPYA

  Saturday, March 18, 2017

  SAMATTA: TUNA UWEZO WA KUING’OA CELTA VIGO ULAYA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba klabu yake inaweza kuitoa Celta Vigo ya Hispania na kwenda Nusu Fainali ya Europa League.
  KRC Genk ya Ubelgiji itamenyana na Celta Vigo ya Hispania katika Robo Fainali ya UEFA Europa League mechi za kwanza zikichezwa Aprili 13 na marudiano Aprili 20, mwaka huu.
  Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online leo, Samatta amesema kwamba Genk watakaoanzia ugenini, wana asilimia sawa, 50 kwa 50 na Celta Vigo katika mchuano huo.
  Mbwana Samatta amesema kwamba Genk wanaweza kuwatoa Celta Vigo na kwenda Nusu Fainali Europa League

  “Celta siyo timu mbaya na wako katika kiwango kizuri kwa sasa, tunategemea mchezo mzuri na mgumu, kwani hata sisi pia tumekuwa katika kiwango kizuri katika mashindano ya Ulaya mwaka huu, kwa hivyo naweza kusema mechi hadi sasa ni 50/50, dakika 180 ndiyo zitakazoamua,”amesema.
  Mechi nyingine za Robo Fainali Europa League ni kati ya Manchester United na Anderlecht ya Ubelgiji, Lyon ya Ufaransa na Besiktas ya Uturuki na Ajax ya Uholanzi na Schalke ya Ujerumani.
  Mechi za kwanza zinatarajiwa kuchezwa Aprili 13 na marudiano Aprili 20.
  Genk imefuzu Robo Fainali ya UEFA Europa League licha ya kulazimishwa sare ya 1-1 na KAA Gent usiku wa Alhamisi Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, kwani ushindi wa 5-2 ugenini katika mchezo wa kwanza unawafanya wasonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 6-3.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA: TUNA UWEZO WA KUING’OA CELTA VIGO ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top