• HABARI MPYA

    Tuesday, March 21, 2017

    SAMATTA, FARID MUSSA WATUA LEO KUJIUNGA NA STARS

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    NAHODHA wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kuwasili nchini leo kuanzia Saa 4:00 usiku kujiunga na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya mchezo ya kirafiki ya kimataifa wiki ijayo.
    Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi mbili, kwanza na Botswana Machi 25 na baadaye Burundi Machi 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na pamoja na Samatta, mchezaji mwingine wa Tanzania anayecheza Ulaya, Farid Mussa anatarajiwa pia kuwasili leo.
    Wakati Samatta anayechezea KRC Genk ya Ubelgiji atatua kwa ndege ya Shirika la Uturuki Saa 4:00 usiku, Farid wa DC Tenerife anatarajiwa kutua kuanzia 9:00 Alfajiri kwa ndege ya KLM.
    Taifa Stars itamkosa mchezaji mwingine wa Ulaya, Thomas Ulimwengu wa AFC Eskilstuna ya Sweden, ambaye hayuko fiti.
    Taifa Stars inaingia kambini leo kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam na kikosi hicho cha kocha Salum Mayanga. 
    Nyota wengine walioitwa Taifa Stars ni walinda milango, Aishi Manula (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
    Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).
    Walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
    Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC).
    Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Hajib (Simba SC), Mbaraka Yussuf (Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).
    Mayanga anasaidiwa kocha wa Makipa, Patrick Mwangata; Meneja wa timu, Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timuatakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa ni Gilbert Kigadya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SAMATTA, FARID MUSSA WATUA LEO KUJIUNGA NA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top