• HABARI MPYA

  Tuesday, March 21, 2017

  OKWI AREJESHWA TIMU YA TAIFA UGANDA BAADA YA KUNG'ARA VILLA

  KOCHA wa Uganda, Milutin Sredojevic 'Micho' ameita wachezaji wa 18 watakaosafiri kwa mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wenyeji, Kenya Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos Alhamisi ndani yake akimrejesha mshambuliaji wa zamani wa Simba na Yanga, Emmanuel Okwi.
  Wachezaji hao waliolala kwenye hoteli ya Sky Hotel, Nalya wanatarajiwa kuondoka Kampala, leo kwenda Nairobi.
  Wachezaji wanaocheza nje wataungana na timu mjini Nairobi.
  Okwi alitemwa kikosi cha The Cranes wakati anacheza SonderjyskE Fodbold ya Ligi Kuu ya Denmark kutokana na kushuka kwa kiwango chake kwa sababu za kutopata nafasi za kuchezeshwa.
  Lakini baada ya kurejea nyumbani kujiunga na SC Villa ya kwao, Okwi ameimarika tena na kurejeshwa kikosini na kocha Micho.
  Kikosi kamili cha The Cranes kinachotarajiwa kuondoka leo Uwanjanwa Ndege wa Entebbe kinaundwa na  makipa;Benjamin Ochan (KCCA), Isma Watenga (Vipers)
  Mabeki: Nico Wakiro Wadad (Vipers), Timothy Denis Awanyi (KCCA), Habib Kavuma (KCCA), Murushid Juuko (Simba, Tanzania), Shafiq Batambuze (Tusker, Kenya), Godfrey Walusimbi (Gor Mahia, Kenya)
  Viungo: Hassan Wasswa Mawanda (Nijmeh, Lebanon), Kirizestom Ntambi (Jimma Aba Buna), Yassar Mugerwa (Saint George, Ethiopia), Moses Waiswa (Vipers), Muzamil Mutyaba (KCCA), Joseph Ochaya (KCCA), Brian Majwega (KCCA)
  Na washambuliaji ni Geofrey Sserunkuma (KCCA), Emmanuel Okwi Arnold (SC Villa) na Milton Karisa (Vipers).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: OKWI AREJESHWA TIMU YA TAIFA UGANDA BAADA YA KUNG'ARA VILLA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top