• HABARI MPYA

  Friday, March 17, 2017

  MKE WA MICHAEL ESSIEN ANUNUA TIMU YA DARAJA LA TATU ITALIA

  MKE wa kiungo wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na Ghana, Michael Essien amenunua timu ya Daraja la Tatu Italia, Como, klabu hiyo imesema jana.
  Akosua Puni Essien ametoa Euro 237 000 katika mnada wa klabu hiyo, kwa muji u wa vyombo vya Habari Italia, baada ya kuthibitisha kufilisika mwaka jana.
  "Tunatarajia mmiliki mpya na timu yake wataziinua timu zote, ya kwanza na ya vijana na kutikisa tena jijini," klabu imesema katika taarifa yake.
  "Watafanya jitihada katika ubunifu wa kuhakikisha wanairejesha timu Serie B na kuendeleza vipaji vya chipukizi wawe bora."
  Michael Essian na mkewe, Akosua Puni Essien sasa ni wamiliki wa timu ya Daraja la Tatu

  Puni Essien amejipambanua kama mfanyabishara wa kike na mtaalamu wa ushauri na mama wa watoto watatu awapendao mno.
  Michael Essien, mwenye umri wa miaka 34, amechezea pia Panathinaikos ya Ugiriki kabla ya Jumatatu wiki hii kuhamia Persib Bandung ya Indonesia.
  Como imewahi kuchea Serie A, kuanzia mwaka 1984 hadi 1989 na baadaye msimu wa 2002-2003 walipoteremka baada ya msimu mmoja.
  Waliteremka hadi Daraja la Tano mwaka 2005 baada ya kufilisika mara ya kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKE WA MICHAEL ESSIEN ANUNUA TIMU YA DARAJA LA TATU ITALIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top