• HABARI MPYA

  Thursday, March 02, 2017

  LUIS ENRIQUE ABWAGA MANYANGA BARCELONA

  Luis Enrique anaamua kupumzika Barcelona baada ya miaka mitatu ya kufanya kazi klabu hiuyo ya Katalunya PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  REKODI YA ENRIQUE AKIWA KOCHA BARCA 

  Kuteuliwa: Julai 2014
  Mechi: 164
  Kushinda: 125
  Sare: 21
  Kufungwa: 18
  Thamani ya ushindi: 76.2% 
  Mataji: La Liga (2015, 2016), Kombe la Mfalme (2015, 2016), Super Cup ya Hispania (2016), Ligi ya Mabingwa (2015), Super Cup ya UEFA (2015), Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA (2015) 
  KOCHA Luis Enrique ametangaza kuondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huku kocha wa Everton, Ronald Koeman akiwa miongoni mwa wanaotarajiwa kumrithi.
  Mholanzi huyo ataondoka miaka 25 baada ya ushindi wake wa Wembley kuipa Barcelona taji la kwanza kabisa la Ulaya.
  Imekuwa siri ya wazi kwamba Enrique hataongeza mkataba mwishoni mwa msimu na ataondoka.
  Uamuzi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 46 kutangaza sasa kuondoka kwake, ni kama kuwaambia wachezaji wake wajitume kumaliza msimu vizuri ili wagane kwa furaha.
  "Nitamalizia mkutano huu na Waandishi wa Habari kwa namna tofauti, nataka kutangaza kwamba sitaendelea kuwa kocha wa Barcelona. Nataka kuishukuru klabu kwa imani yao yote waliyoonyesha kwangu. Hiyo imekuwa miaka mitatu ya kutosahaulika,"alisema jana baada ya ushindi wa 6-1 dhidi ya Sporting Gijon jana.
  Ushindi huo umeirejesha Barca kileleni mwa La Liga, ikifikisha pointi 57 baada ya mechi 25 na kuashushia nafasi ya pili, Real Madrid yenye pointi 56 za mechi 24 sasa baada ya sare ya 3-3 na Las Palmas jana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LUIS ENRIQUE ABWAGA MANYANGA BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top