• HABARI MPYA

  Thursday, March 02, 2017

  RONALDO AINUSURU REAL MADRID KUPIGWA NYUMBAN LA LIGA, BALE ALIMWA NYEKUNDU

  Cristiano Ronaldo akiruka juu kuifunia bao la kusawazisha Real Madrid dakika ya 89 katika sare ya 3-3 na Las Palmas kwenye mchezo wa La Liga usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu. Ronaldo alifunga mabao mawili jana, lingine kwa penalti dakika ya 86, wakati bao lingine la Real Madrid iliyompoteza winga wake, Gareth Bale aliyetolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 47, lilifungwa na Isco dakika ya nane na ya Las Palmas yalifungwa na Tana Dominguez dakika ya 10, Jonathan Viera kwa penalti dakika ya 56 na Kevin-Prince Boateng dakika ya 59. Kwa matokeo hayo, Real inaangukia nafasi ya pili kwenye msimamo wa La Liga kwa pointi zake 56 za mechi 24, ikiipisha juu Barcelona yenye pointi 57 za mechi 25 PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AINUSURU REAL MADRID KUPIGWA NYUMBAN LA LIGA, BALE ALIMWA NYEKUNDU Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top