• HABARI MPYA

  Saturday, March 18, 2017

  KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA MADINI 5,000

  Na Clement Shari, ARUSHA
  KIINGILIO cha chini katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baina ya wenyeji, Madini FC na Simba SC kesho Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha kitakuwa ni Sh. 5,000.
  Katibu wa Chama cha Soka Arusha (ARFA), Zakayo Mjema ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online jana kwamba maandalizi yote muhimu kuelekea pambano hilo yameshakamilika.
  Mjema ametaja viingilio vingine kuwa ni Sh 20,000- VIP A, wakati wale watakaoketi VIP B1 na VIP B2 watalipa Sh 7,000 na Sh 5,000 itakuwa kwa jukwaa la VIP C1 na VIP C2.
  Mjema amesema tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Jumapili kuanzia saa moja  
  asubuhi Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na kwamba hakuna gari lolote litakaloruhusiwa kuingia uwanjani siku ya mchezo, hivyo wapenzi wa soka watakaokuwa na magari  
  watalazimika kutafuta maegesho nje ya Uwanja.
  Timu hizi zinakutana kwa mara ya kwanza kabisa katika historia ya soka la Tanzania, Madini wanashiriki Ligi Daraja la Pili wakati Simba ni vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa sasa. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KIINGILIO CHA CHINI SIMBA NA MADINI 5,000 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top