• HABARI MPYA

    Thursday, March 02, 2017

    GSM MBIONI KUINUNUA AFRICAN LYON

    Na Mwandishi Wetu, DAE ES SALAAM
    KAMPUNI ya GSM Limited iko mbioni kuinunua klabu ya African Lyon ya Dar es Salaam baada ya kushindwa kumilikishwa Maji Maji ya Songea.
    Mazungumzo kati ya uongozi wa GSM chini ya Mkurugenzi wake Mkuu, Ghalib Mohammed na African Lyon yanaendelea na inaelezwa yamefikia pazuri na wakati wowote dili hilo linawezwa kuwekwa wazi.
    Rahim Kangezi ‘Zamunda’, mmiliki wa Lyon yuko tayari kuikabidhi timu hiyo kwa wamiliki wapya, GSM baada ya yeye kuinunua kwa ‘bei chee’ mwaka 2010 kwa Mohammed Dewji, ambaye naye aliinunua mwaka 2007 kwa wafanyabiashara wa soko la Mbagala, enzi hizo ikiitwa Mbagala Market.
    Mkurugenzi Mkuu wa GSM inayotaka kuinunua African Lyon, Ghalib Mohammed 

    Na GSM wanataka kuinunua Lyon baada ya mpango wa kutaka kumilikishwa Maji Maji kushindikana kutokana na wanachama wa klabu hiyo kukataa. Kwa sasa GSM ni wafadhili wa Maji Maji ya Ruvuma, mkoa ambao anatokea Ghalib.
    Kwa kuwa GSM sasa wanaamua kuwekeza kwenye soka, wakiwa na mpango wa kumiliki klabu kubwa hapa nyumbani mithili ya Azam FC, yenye Uwanja wake, akademi na kujiendesha kisasa – wanalazimika kununua timu nyingine.
    “Mazungumzo na Lyon yanaendelea, wakati wowote mipango ikikaa sawa itatangazwa hadharani, kwa sasa bado,”kimesema chanzo kutoka GSM.  
    Habari zaidi zinasema kwamba GSM wanasubiri kuona kama African Lyon itabaki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara ndiyo waweze kufanya biashara hiyo.
    Kwa sasa Lyon ipo nafasi ya 13 katika msimamo wa Ligi Kuu ya timu 16 ikiwa na pointi 22 za mechi 23 na bado ina kibarua cha kupigana kuhakikisha inakuwa nje ya timu ya timu tatu za chini zitakazoshuka Daraja kuzipisha Lipuli ya Iringa, Mji ya Njombe na Singida United ya Singida zilizopanda kuelekea msimu ujao.     
    Iko juu ya Toto African ya Mwanza, Maji Maji zenye pointi 22 za mechi 23 pia kila moja na JKT Ruvu yenye pointi 20 za mechi 24. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: GSM MBIONI KUINUNUA AFRICAN LYON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top