• HABARI MPYA

  Sunday, March 19, 2017

  AZAM FC HADITHI IMEKWISHA MAPEMAA AFRIKA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  AZAM FC imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika baada ya kufungwa mabao 3-0 na wenyeji Mbabane Swallows jioni ya leo nchini Swaziland.
  Kulikuwa kuna vitendo visivyo vya kiungwana kabla ya mchezo, ikiwemo Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba kupigwa na mashabiki mbele ya Polisi.
  Lakini mbaya zaidi, wachezaji wa Azam walishindwa kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwa madai wenyeji walivipulizia dawa kali ya sumu.
  Kiungo wa Azam FC, Frank Domayo akiurukia mpira wa juu katikati ya wachezaji wa Mbabane Swallows

  Bado haikusaidia, kikosi cha Azam FC kilipoingia uwanjani kikatandikwa mabao 3-0 na hivyo kutolewa kwa jumla ya mabao 3-1, baada ya ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Dar es Salaam wiki iliyopita.
  Azam FC sasa itabidi ielekeze nguvu zake kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) ili kurejea kwenye michuano ya Afrika mwakani.
  Na hiyo inatokana na kuachwa mbali na vinara Simba SC na mabingwa watetezi, Yanga SC kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Tayari Azam FC ipo Robo Fainali ya Kombe la ASFC na itamenyana na Ndanda FC kujaribu kuzifuata, Mbao FC ya Mwanza, Simba, na ama Yanga au Prisons katika Nusu Fainali.
  Kikosi cha Azam leo kilikuwa; Aishi Manula, Shomari Kapombe, Bruce Kangwa, Daniel Amoah, Yakubu Mohammed, Erasto Nyoni, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Himid Mao, Yahaya Mohammed/Joseph Mahundi dk80, Frank Domayo na Ramadhan Singano ‘Messi’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC HADITHI IMEKWISHA MAPEMAA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top