• HABARI MPYA

    Saturday, March 04, 2017

    MIKAKATI YA AHMAD AKIFANIKIWA KUMNG'OA HAYATOU CAF

    MGOMBEA Urais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad amesema kwamba atafanya mageuzi makubwa katika soka barani akifanikiwa kumng'oa Rais wa muda mrefu, Issa Hayatou.
    Ahmad, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF na kiongozi mkuu wa Shirikisho la Soka Madagascar amefanya ziara ya mwisho ya kampeni nchini Nigeria kuelekea uchaguzi wa CAF Machi 16 mjini Addis Ababa, Ethiopia.
    "Nafikiri mambo mengi yanatakiwa kubadilika katika soka ya Afrika", amesema Ahmad.
    Ahmad Ahmad anataka kufanya mageuzi makubwa katika soka barani akifanikiwa kumng'oa Issa Hayatou

    Tunahitaji mabadiliko katika urefa, uchezeshaji, namna tunavyowafundisha makocha wetu. Hatuwezi kuandaa kozi ya leseni ya kwa siku 15 na 10. Cheti kinakufanya wewe upate kazi. Miradi yetu ya maendeleo lazima ibadilike,"amesema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MIKAKATI YA AHMAD AKIFANIKIWA KUMNG'OA HAYATOU CAF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top