• HABARI MPYA

    Tuesday, November 01, 2016

    SIMBA, YANGA WAANZA KUMTOA JASHO MZEE EL-MAAMRY SUALA LA KESSY

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    MSULUHISHI wa kisheria wa sakata la madai ya Simba dhidi ya Yanga na mchezaji Hassan Kessy, Wakili Said Hamad El-Maamry anatarajiwa kukutana na pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili kufikia mwafaka wa mwadai hayo.
    Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji iliagiza pande za Simba na Yanga kumaliza suala hilo mapema mwezi uliopita, lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na Kamati yake walishindwa kufanya hivyo kupewa barua ya wito kuitwa kikaoni Oktoba 29, mwaka huu.
    Hata hivyo, msuluhishi huyo alishindwa kuendelea na kikao hicho baada ya taarifa kutoka Yanga kusema kwamba mmoja wa Wawakilishi wake, Wakili Msomi Alex Mgongolwa kuwa safarini Iringa alikokwenda kwa sababu ya matatizo ya kifamilia. 
    Ilielezwa kuwa Mgongolwa ambaye ni Mwanasheria wa Yanga alifiwa hivyo kuomba kupangiwa siku nyingine.
    Kutokana na hali hiyo, E-Maamry amepanga sasa kukutana nna viongozi na/ au Wawakilishi wa pande zote mbili Alhamisi saa 11.00 jioni kwenye ofisi za TFF ili kuketi chini ya kuangalia namna ya kumaliza madai ya Simba iliyowasilisha mashauri mawili ambako moja ni dhidi ya Yanga ilihali jingine ni dhidi ya mchezaji Hassan Kessy.
    Said El Maamry (kulia) akimkabidhi tuzo yake ya Refa Bora wa Ligi Kuu, Ngole Wangole (kushoto) 

    Mzee El-Maamry amesema: “Ili kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa pande zote kusikiliszwa. Ni vema Mwanasheria wa Yanga akasubiriwa.”
    Kamati ya TFF inasuburi makubaliano hayo, na ikitokea imeshindikana, suala hilo litarudi kwenye Kamati hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria zinazoongoza mpira wa miguu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA, YANGA WAANZA KUMTOA JASHO MZEE EL-MAAMRY SUALA LA KESSY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top