• HABARI MPYA

    Wednesday, November 02, 2016

    JUUKO AITWA UGANDA MECHI YA KOMBE LA DUNIA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KOCHA Mserbia wa timu ya taifa ya Uganda, Miliutin Sredojevic ‘Micho’ amemuita beki wa Simba Juuko Murshid katika kikosi cha wachezaji 19 kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa mwezi huu.
    Uganda itamenyana na Zambia Novemba 8 kabla ya kumenyana na Kongo Brazzaville Novemba 12 Uwanja wa Taifa wa Mandela, Namboole katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia.
    Na Micho ameita wachezaji 19 wanaocheza nje ambao baadaye wataunganishwa na wacheaji 11 wa nyumbani kupata jumla ya nyota 30 watakaojiandaa na mchezo huo.
    Beki wa Simba Juuko Murshid ameitwa kwenye kikosi cha wachezaji 19 wa Uganda kwa ajili ya mechi mbili za kimataifa mwezi huu

    Akizugumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE kwa simu kutoka Kampala, Uganda leo, Micho alisema kwamba amemjumuisha Juuko katika kikosi chake baada ya kufuatilia maendeleo yake katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. “Ninajua anafanha vizyri, kwa sasa anacheza na maana yake atakuwa vizuri zaidi,”alisema Micho ambaye anasaidiwa na Kocha wa zamani wa Simba, Moses Basena.
    Kikosi kamili cha wachezaji wa kigeni kilichotajwa na Micho ni makipa; Denis Onyango, Robert Odongkara na Salim Jamal Magola, mabeki; Denis Iguma, Walusimbi Godffrey, Isaac Isinde, Murshid Juuko, Ronald Mukiibi na Mike Azira
    Viungo; Shafic Batambuze,Godffrey Baba Kizito, Tonny Mawejje, Yassar Mugerwa, Moses Oloya na Khalid Aucho wakati washambuliaji ni Faruku Miya, Yunus Sentamu, William Kizito Luwagga na Geoffrey Massa.
    Wachezaji 22 wa nyumbani walioitwa ambao kati yao 11 wataungana 19 wa kigeni kupata idadi ya wachezaji 30 watakaojiandaa na mchezo huo ni makipa; Benjamin Ochan na Ismail Watenga, mabeki; Nicholas Wadada, Denis Okot , Joseph Nsubuga, Hassan Wasswa, Joseph Ochaya, Kasagga Richard , Awanyi Timoth na Halid Lwaliwa.
    Viungo ni Muzamil Mutyaba, Kizito Keziron, Sadam Juma, Shafic Kajimu,Lwesibawa Godffrey, Kayiwa Allan, Vitalis Tabu na Abdul Malik, wakati washambuliaji ni Muhammad Shaban, Geoffrey Serunkuma, Edrisa Lubega, Erisa Sekisambu na Derrick Nsibambi.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: JUUKO AITWA UGANDA MECHI YA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top